Msanii wa
bongo fleva nchini Abdul Chende ‘Dogo Janja, ameachia kibao chake kipya kinachoitwa
natoa ya moyoni ikiwa ni rekodi yake ya kwanza chini ya usimamizi wa Ustadh Juma mwenye kundi
la Mtanashati ambaye alimchukua kukiendeleza kipaji chake.
Dogo Janja
ambaye awali alikuwa akifanya kazi na Kundi la Madee, alisema kibao hicho
amemshirikisha PMC na amerekodi kwa Michael Chali .
Alisema “Nashukuru
Mungu mtanashati wamenisaidia nimerekodi wimbo kwani kuna watu walidhani kwamba
siwezi tena kuendelea kuimba lakini Mungu yupo pamoja name, ninaendelea kama
kawa,”
Msanii huyo
alikwaruzana na Madee siku za karibuni, na hivyo kurudishwa kwao Arusha, ambapo
Mtanashati aliona amchukue ili kipaji chake kisipotee.
Dogo Janja alisema
hana kinyongo na Madee na anashukuru kwa kumfanya ajulikane kwa vile kama sio
yeye pengine asingejulikana, lakini zaidi alimshukuru Tunda man kwa kutoonyesha
kinyongo kwake.
No comments:
Post a Comment