Kwa mujibu
wa taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Kampuni hiyo Kelvin
Twissa inaeleza kuwa mashindano hayo yatakuwa katika awamu mbili, awamu ya
kwanza hapa nchini na washindi kushiriki mashindano ya pili nchini Afrika
Kusini.
Alisema kuwa washiriki wataangalia mahitaji ya
watanzania na kutengeneza Programu inayofaa ambayo itatumiwa na jamii kama
zinavyotumika Google au mtandao wa kijamii wa Facebook ambayo itamnufaisha
mtengenezaji na kubadilisha maisha yake itakapoanza kutumika.
Twissa alisema
mashindano yameanzishwa ili kuwapa motisha vijana ambao wanaendeleza ubunifu wa
kiteknolojia katika simu, hivyo shindano linatoa nafasi kwa washiriki kuonesha
uwezo wao katika kuvumbua vifaa mbalimbali vinavyoweza kutumika katika nchi
zinazoendelea na kutatua matatizo yanayoikumba jamii.
Alisema
washindi watakaopatikana katika mashindano ya awali ndani ya nchi shiriki
ambazo ni Tanzania, Misri, Lesotho, Afrika Kusini na Qatar watapata nafasi ya
kushiriki katika mashindano ya kimataifa Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka huu
na kuongeza Mshindi wa hapa nchini Vodacom itamdhamini kushiriki mashindano ya
kimataifa.
Alisema katika
mashindano ya ndani washiriki wanatakiwa kuendeleza ubunifu katika vipengele
mbalimbali kama michezo, afya ya jamii, burudani na simu. Mshindi mmoja katika
kipengele atapata dola 2000 za Marekani, na baada ya hapo kwa mshiriki ambaye
atakuwa ametoa program bora atapata nafasi ya kushiriki katika michuano ya
kimataifa.
Kwa mujibu
wa Twissa ni kwamba maombi yatawekwa na kusambazwa kupitia hifadhi ya program
ya Vodacom na Vodafone na watu binafsi kuendelea kukusanya hadi mwisho wa muda
wa kuwakilisha.
Alisema
Vodacom kama muasisi wa mashindano hayo yaliyopewa jina la Appstar Challenge,
inaalika washiriki kuzichapisha program zao kwenye hifadhi ya Vodacom au waende
ofisi za Kinu ambapo mwisho wa shindano ni Septemba 3 mwaka huu.
Twissa
alibainisha kuwa katika mashindano ya kimataifa, program mbili zitakazoshinda
zitapelekwa katika mchujo wa wataalamu wa kimataifa kutoka Vodacom na washiriki
wataonesha kazi zao mbele ya majaji hao kwa vitendo.
No comments:
Post a Comment