Na Mwandishi Wetu
MAMBO yanazidi
kumnyookea mwanamitindo nyota wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata baada
ya kuingia mkataba wa kutangaza nguo za kampuni inayoongoza nchini Afika
Kusini na Mashariki ya Kati, Truworths.
Kampuni ya Truworths
inaongoza kwa kuuza nguo za jumla na rejareja siyo Afrika Kusini ambapo kuna
maduka ya kuuza na kusambaza zaidi ya 400 na kuwapa kibali cha
kufanya biashara hiyo katika nchi 14 za Mashariki ya Kati (Middle East)
na Afrika.
Hatua ya Flaviana
kupata nafasi hiyo imetokana na jina lake katika masuala ya maonyesho mbali mbali
ya mitindo katika nchi hiyo, Uingereza na Marekani ambako ndiko anafanyia kazi
kwa sasa.
Flaviana ambaye pia
ni Miss Universe wa mwaka 2007, ameweza kutangaza nchi nje ya mipaka yake
kupitia masuala ya maonyesho ya mavazi na kwa sasa anaishi nchini Marekani kwa
kufanya shughuli hiyo.
Kuingia mkataba kwake
katika kampuni hiyo kutampa nafasi kubwa ya kuinadi Tanzania kwani ni
mwanamitindo pekee ambaye amepata nafasi hiyo kubwa nay a kujivunia.
Akizungumzia nafasi
hiyo, Flaviana alisema kuwa anashukuru Mungu kwa kupata mikataba mingi ya
kufanya kazi za matangazo hasa kupitia mitindo kwa kampuni kubwa kama vile
Diesel na Edun.
“Ni faraja
kubwa kupata mikataba hii nah ii inatokana na juhudi zangu za na
mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai za kwa kuniongoza
vyema, mpaka sasa nimeweza kushiriki katika matukio mengi ya kimataifa nje ya
Tanzania na hasa katika nchi za Marekani na Uingereza,” alisema Flaviana.
Alisema kuwa
kazi ya kuonyesha mitindo si kazi rahisi na ndiyo maana si kila msichana au
mvulana anaweza kufanya kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment