Wednesday, 29 May 2013
Lady Jaydee ameahirisha tamasha lake
Kufuatia kifo cha msanii wa Hip Hop nchini Albert Mangwea aliyefariki jana nchini Afrika ya Kusini, Msanii mkongwe wa Tanzania Judith Wambura Lady Jaydee ameahirisha tamasha lake la 13 lililokuwa lifanyike Mei 31, Nyumbani Lounge.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Lady Jaydee amewaomba radhi mashabiki wake na kuwaeleza kuwa wawe wavumilivu hadi msiba wa msanii mwenzao utakapokwisha.
Alisema baada ya msiba kiusha atatangaza tena ni lini afanye tamasha hilo.
Wasanii wengine ambao nao walikuwa wafanye tamasha hilo mwishoni mwa mwezi huu ni Mwana FA, Kalapina na Izzo Buziness ambao nao wameahirisha kufuatia msiba huo wa msanii mwenzao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment