Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga akizungumza na warembo |
Na Mwandishi Wetu
Nani
kutwaa taji la Redds Miss Sinza leo? Jibu la swali hilo litajulikana
leo wakati warembo 12 wanaowania taji la hilo watakapopanda jukwaani
kwenye ukumbi wa Meeda Club kushindania taji hilo.
Mashindano
hayo ambayo yamepangwa kuanza saa 1.00 usiku, yatashuhudia Redds Miss
Tanzania, Brigitte Alfred akivua taji lake la kwanza katika usiku huo
ambao utakuwa na buudani za kila aina. Mbali ya kuwa Miss Sinza,
Brigitte pia anashikilia taji la Redds Miss Tanzania.
Mbunifu
wa mitindo anayekuja juu kwa kasi, Veronica Lugenzi atanogesha shindano
hilo kwa kuwavalisha nguo za mitindo mbali mbali warembo. Veronica ni
mmoja wa wabunifu maarufu wa mitindo na ameahidi kuwapendezesha warembo
wote katika usiku huo wa burudani.
Warembo
wataanza kwa kucheza shoo ya ufunguzi na baadaye kupita jukwaani wakiwa
wamevalia mavazi ya ubunifu, ufukweni na baadaye usiku kabla ya kujibu
maswali kwa watakao ingia tano bora.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema jana kuwa maandalizi yamekwisha kamilika na bendi namba
moja nchini, African Stars “wana Twanga Pepeta’ itatumbuiza siku kwa
mara ya kwanza na kutoa zawadi kwa wakazi wa Sinza na vitongoji vyake.
Majuto
alisema kuwa bendi hiyo itatambulisha nyimbo mpya ambazo
zitatambulishwa rasmi katika uzinduzi uliopangwa kufanyika Juni 30
kwenye viwanja vya Leaders Club.
“Ikumbukwe
kuwa twanga pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na wameandaa
zawadi maalum kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyo dhaminiwa
na Redds Original, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito
Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group, Salut5.com na Sufiani
Mafoto blog,” alisema Majuto.
Alisema kuwa nyimbo mpya kama Nyumbani ni Nyumbani, Ngumu Kumeza, Shamba la Twanga na nyimbo nyingine nyingi zitatambulishwa katika mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment