Kombe hilo likiandaliwa kwa ajili ya kukabidhiwa NSSF ALL STARS |
Kikosi cha wanahabari |
Kikosi cha wanahabari na Wabunge |
Na Mwandishi wetu
TIMU inayoundwa na wachezaji kutoka
vyombo vya habari mbali mbali vilivyoshiriki katika michuano ya NSSF “NSSF
Media All Stars” imevunja mwiko wa timu ya Bunge FC ya kutofungwa kwa miaka
tisa baada ya kuichapa kwa bao 1-0.
Katika mchezo huo uliofanyika Jumamosi
kwenye uwanja wa Jamhuri na kuhudhuriwa na watazamaji wengi katika historia ya
uwanja wa Jamhuri, ulikuwa mkali na wa kusisimua na timu zote zilishambuliana
kwa zamu.
NSSF all Media ilianza mchezo huo
kwa kasi kufanya mashambulizi makali katika dakika 10 za kwanza.
Julius Kihampa
alikosa bao la wazi katika dakika ya pili baada ya pasi safi kutoka kwa
Mbozi Katala ambaye alishirikiana vyema na Maulid Kitenge, Wilbert Molandi na
Emmanuel China.
Dakika ya saba, shuti la faulo
iliyopigwa na nahodha wa timu hiyo, Majuto “Ronaldo” Omary iligonga mwamba
baada ya kumshinda kipa wa Bunge FC Idd Azzan ambaye hakuweza kufanya lolote.
NSSF all Media ilisheherekea bao
lake pekee katika dakika ya tisa kwa kichwa kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na
Majuto ambaye aliwatoka walinzi wawili kutoka upande wa kulia na kupiga krosi
safi.
Bunge FC ilijikuta ikiutafuta
mpira kwa tochi muda mwingi, ilishindwa kufanya mashambulizi ya kina karibu
dakika 70 na kuifanya NSSF all Media Stars iliyokuwa chini ya kocha wake,
mchezaji wa zamani wa mabingwa wa soka nchini Yanga, Sanifu Lazaro
ilitawala muda mwingi.
Baada ya goli hilo Bunge FC
walijitahidi kushambulia lakini ngome ya NSSF Media Cup Stars FC chini ya kipa
Said Ambua ilikuwa imara kuokoa hatari zote langoni.
Katika mechi ya wanawake, Bunge
Quuens iliyokuwa ikiongozwa na Halima Mdee (GK) na Esta Bulaya (WD) ilitoka
kifua mbele kwa magoli 31 kwa 18 ya NSSF Media Cup Stars Queens.
Katika mechi hiyo iliyoshuhudiwa na
mawaziri mbalimbali pamoja na huku mgeni rasmi akiwa Naibu Spika
wa Bunge Job Ndugai, Bunge Queens
ilikuwa ikiongoza kwa magoli 17-10.
Magoli ya NSSF Media Cup Stars
Queens yalifungwa na Lulu Habib na Imani Makongoro (GS) aliyemtoa jasho halima
Mdee (GK).
Baada ya mechi hiyo Naibu Spika, Job
Ndugai alizipongeza timu za kombaini za NSSF hasa ya soka ambayo imeweka
rekodi mpya kwa kuwafunga wabunge kwenye uwanja wao.
“ Mmeonyesha uwezo mzuri lakini pia
mmeonyesha kweli nyie ni wachezaji makini kwani mara kwa mara wabunge
hawafungwi hapa Dodoma lakini nyinyi mmekuwa wa kwanza hongereni sana,"
alisema Ndungai ambaye ndiye alikabidhi vikombe kwa washindi kwa kushirikiana
na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, DK Ramadhan Dau.
No comments:
Post a Comment