Professa Jay kushoto akiwa na mama yake mzazi |
MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Joseph Haule maarufu kama Professa Jay amesema mama yake mzazi anatarajiwa kuzikwa Kesho Jumapili kwenye makaburi ya Kinondoni.
Mama wa
msanii huyo maarufu kama mama Majanjala alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi
baada ya kugongwa na gari aina ya starlet wakati alipokuwa akivuka barabara katika
eneo la Mbezi mwisho ambapo ndiko yaliyoko makazi ya Professa Jay.
Akizungumz na gazeti hili, Professa Jay alisema mama yake
alikuwa na utamaduni wa kutoka wakati wa usiku kwa ajili ya mazoezi kwasababu alikuwa akichoka mchana kutwa kutokana na
kutofanya shughuli zozote.
“Mama yangu alikuwa na utamaduni wa kutoka
kila siku jioni kwa ajili ya kutembea tembea kama sehemu ya mazoezi, sasa juzi
wakati anatoka ndipo alipogongwa,”alisema.
Alisema mara
baada ya dereva wa gari hiyo ya starlet kumgonga mama yake Professa Jay,
alimchukua na kwenda kuchukua PF3 na kumkimbiza katika hospitali ya Tumbi
Kibaha kwa ajili ya matibabu lakini hakukaa muda mrefu akapoteza maisha.
Professa Jay
alisema msiba upo nyumbani kwake Mbezi mwisho na shughuli zote zitafanyika
kwake, kisha mama yake huyo kuzikwa Jumapili.
Mama huyo
aliwahi kufanya kazi kwenye Benki ya Posta Tanzania kama mtawala (administrator)
ambapo alistaafu rasmi mwaka 2010.
Mungu ailaze
roho ya mama Mwanjala mahali pema peponi
na tunawapa pole Professa Jay na ndugu zake kwa kufiwa na mama yao.
No comments:
Post a Comment