Na
Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amewataka watu wenye
ulemavu kutoa maoni yao kuhusu rasimu ya katiba ili kuiwezesha Tume yake kujua
mahitaji yao na kuyafanyia kazi.
Akizungumza
katika siku ya kwanza ya mkutano wa Baraza Maalum la Katiba kwa ajili ya watu
wenye ulemavu mjini Dodoma leo (Alhamisi, Agosti 15, 2013), Jaji Warioba
amesema Tume yake inatarajia kupata maoni mazuri yanayohusu watu wenye ulemavu
kutoka katika baraza hilo.
“Mtusaidie
kupata maoni kuhusu maeneo yote ya rasimu ya katiba yanayohusu watu wenye
ulemavu,” alisema na kuongeza kuwa hilo lisiwazuie kutoa maoni kuhusu maeneo
mengine ya rasimu ya katiba.
“Nyie
pia ni sehemu watanzania na hata mkiwa viongozi mtakuwa viongozi wa watanzania
wote... kwa hiyo ipitieni rasimu yote na mtoe maoni katika maeneo yote pia,”
alisisitiza Jaji Warioba na kuongeza kuwa Tume yake pia iliandaa Baraza Maalum
kama hilo Zanzibar kwa kushirikiana na Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar
(UWZ).
Akiongea
katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Shirikisho la Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA),
Bw. Novatus Rukwago aliishukuru Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwezesha
kufanyika kwa baraza hilo na kusema kuwa mkutano huo umeshirikisha vyama vyote kumi
vya watu wenye ulemavu.
Alivitaja
vyama hivyo kuwa ni Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (CHAWATA), Chama cha
Wasiiona (TLB), Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Afya ya Akili (TUSPO) na Chama
cha Watu Wenye Ulemavu Walioumia Uti wa Mgongo Kilimanjaro (KASI).
Vyama
vingine vinavyohudhuria mkutano huo ni Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA),
Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Mabaka ya Ngozi (PSORATA), Chama cha Albino
Tanzania (CAT), Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Akili (TAMH), Chama cha Viziwi
Wasioona (TASODEB) na Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Vichwa Vikubwa na Mgongo
Wazi (ASBAHT).
Kuhusu Gharama za
Muungano
Katika
hatua nyingine, Jaji Warioba amefafanua kuhusu gharama za uendeshaji wa
muungano wa shirikisho la Serikali tatu ambao umependekezwa na Tume yake katika
rasimu ya katiba iliyozinduliwa Juni 3 mwaka huu.
Akijibu
swali la mjumbe mmoja wa Baraza hilo aliyeomba ufafanuzi kuhusu gharama za
uendeshaji wa Serikali ya Muungano ndani ya shirikisho, Jaji Warioba amesema
Tume yake imependekeza Serikali ya Muungano iendeshwe na mapato yatakayotokana
na ushuru wa bidhaa ambao unakua kila mwaka.
“Tumependekeza
chanzo hiki kikubwa cha ushuru wa bidhaa baada ya kupokea maoni ya wataalam na
kujiridhisha,” alisema na kufafanua kuwa mapato yanayotokana na ushuru wa
bidhaa yanatosha kuendesha shughuli za Serikali ya Muungano inayopendekezwa.
Akiongea
kuhusu suala hilo katika mkutano huo, Mjumbe mwingine wa Tume hiyo Bw. Ally
Saleh amesema kwa sasa mapato ya ushuru wa bidhaa ni zaidi shilingi trilioni
moja na kuwa maoni ya wataalam ambayo Tume yake imeyapokea yanaonyesha kuwa kwa
kiasi kikubwa mapato hayo yanakua kila mwaka.
“Kwa
hiyo mapato haya ya ushuru wa bidhaa yanatosha kuifanya Serikali ya Muungano
ijisimamie na mapato mengine waachiwe washirika wa Muungano,” amesema.
Mkutano
huo wa Baraza Maalum la Watu Wenye Ulemavu unamalizika kesho (Alhamisi, Agosti
16, 2013). Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaendelea na mikutano ya Mabaraza ya
Katiba ili kupokea maoni kuhusu rasimu ya katiba. Mikutano hiyo inatarajia
kumalizika
No comments:
Post a Comment