Na Mwandishi wetu
MKAZI
wa Kigoma, Abdallah Aly Ngagari (51) ameshinda gari aina ya Vitz
iliyoendeshwa na kampuni ya Push Mobile Media ya kunogesha tamasha la
Fiesta.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka Kigoma, Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile
Media, Rugambo Rodney alisema kuwa tayari Ngagari amekabiziwa gari yake
katika hafla fupi iliyofanyika huko huku Kigoma.
Rugambo alisema kuwa baada ya kukamilisha bahati nasibu hiyo, kwa sasa nguvu zao wanazielekeza mkoani Tabora katika tamasha la Fiesta ambalo litafanyika Ijumaa.
Alisema
kuwa watatoa pikipiki kwa wapenzi wa muziki wa Tabora ambapo ili
kushinda, mashabiki wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili
kushinda pikipiki au fedha taslim shs 100,000.
“Tumepania
kutoa zawadi katika mikoa yote ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga
zaidi ya sh milioni 80 ili kufanikisha zoezi hili ambapo magari aina ya
vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki, tunawaomba mashabiki
kushiriki kwa nguvu zote,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa wamejipanga kufanya zoezi hilo na lengo kubwa ni kuwazawadia mashabiki wao ambao na kufaidika na tamasha hilo.
Kwa
mujibu wa Rugambo, zawadi zote zipo katika mikoa ambayo fiesta
imefanyika na ndiyo maana wameweza kutoa zawadi mkoani Kigoma mara baada
ya kuchezesha droo.
No comments:
Post a Comment