![]() |
Kenny Ngomuo |
Na Mwandishi wetu
MTANDAO wa
Jinsia Tanzania (TGNP) imekutana na wananchi wa Mwananyamala wapato 50 kuchambua rasimu ya
katiba.
Mwanaharakati wa TGNP Kenny Ngomuo ameiambia Blogu ya jamii kuwa lengo la
kukutana na wananchi ni kutaka kujenga uelewa wa pamoja wa masuala ya Katiba.
Alisema TGNP
imeona iwashirikishe wananchi katika kuchambua mapungufu yaliyopo, kwa lengo la
kupata mapendekezo na maboresha ya
katiba rasimu kwa manufaa ya wanawake wote.
“Tumeanza
kuchambua rasimu ya katiba na leo tuko Mwananyamala, tunaamini kwamba kwa
mawazo ya pamoja tunaweza tukapata
maboresho na mapendekezo yatakayoingizwa kwenye katiba mpya, ili kuwasaidia
wanawake kupata haki zao,”alisema Ngomuo.
Alisema TGNP
itahakikisha wanawake walioko pembezoni
wanatoa sauti zao kwasababu ndio wazalishaji wakubwa.
“Tutahakikisha
wanawake walioko pembezoni wanashiriki kikamilifu kwasababu ndio ambao hukumbwa
na mfumo kandamizi, ni wazalishaji lakini hawapati haki ya kumiliki rasilimali
ardhi,”alisema.
Alisema katika
uchambuzi wao, baadhi ya mambo waliyoyapendekeza kabla ya kutolewa kwenye
rasimu ya katiba mpya, baadhi yapo ingawa yana mapungufu machache.
Akatolea mfano
haki za wanawake limeingizwa lakini halijawekwa kwenye misingi wa haki za
binadamu, hivyo bado wataendelea kulipigia kelele ili hatimaye liingizwe.
Haki za
wanawake kumiliki rasilimali ardhi, anadai kuwa halijaingizwa kwenye misingi,
kwani nalo linahitaji liingizwe huko, kuwapa nafasi ya haki na ulinzi wa
shughuli zao za uzalishaji
No comments:
Post a Comment