Na Mwandishi wetu,
Igunga.
Jeshi la Polisi wilaya ya
Igunga mkoani Tabora linamshikilia Bw.Msengi Daudi(33)mkazi wa kitongoji cha Mwayunge mjini Igunga kwa tuhuma ya mauaji.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi
wilayani hapa lilisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 5:00 usiku
katika kilabu cha pombe za kienyeji cha Gelesoni kilichopo mjini Igunga.
Lilisema kuwa mtuhumiwa huyo alimchoma kisu mgongoni Bi.Happiness Joseph(45)mkazi
wa Mwayunge mjini Igunga.
Nae Mwenyekiti wa
kitongoji hicho Bw.Ally Isike alikiri kutokea kwa tukio
hilo na kulaani kitendo hicho kuwa ni cha kinyama.
Alisema kuwa mwanamke huyo
alikuwa akiuza pombe za kienyeji aina ya wanzuki kilabuni hapo ambapo baadaye
kulizuka ugomvi baina yake na mtuhumiwa kitendo kilichopelekea mtuhumiwa
kumchoma kisu mgongoni.
Aliongeza kuwa baada ya kuchomwa kisu alipelekwa katika
Hospitali ya wilaya ya Igunga kwa matibabu ambapo hali ilizidi kuwa mbaya na
hatimaye kupoteza maisha.
“Nimepokea taarifa hii kwa
masikitiko makubwa sana,tukio hili ni la kwanza kutokea katika kitongoji
hiki,kitendo hiki kwakweli ni cha kikatili na unyama mkubwa hakipaswi
kuvumiliwa, naomba sheria ifuate mkondo wake”.Alisema Isike.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Peter Ouma alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina ya mtuhumiwa na
marehemu unaodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
No comments:
Post a Comment