Na Mwandishi wetu,
Igunga.
Watu 11 wanaodaiwa kuwa ni
wahamiaji haramu wamenaswa na Jeshi la Polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizotolewa na jeshi hilo zinasema kuwa wahamiaji hao haramu walinaswa katika
juhudi za oparesheni iliyoanzishwa na kikosi cha usalama barabarani ambapo
walifanikiwa kuwakamata watu hao.
Aidha jeshi hilo la Polisi
lilisema kuwa wahamiaji hao haramu walikamatwa Septemba 13 mwaka huu majira ya
saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha mgongoro kata ya Igunga wilayani hapa na
kikosi cha usalama barabarani ambacho kilikua kinaongozwa na mkuu wa kikosi
hicho wilaya ya Igunga Bw.Ame Alawi.
Jeshi hilo la polisi
liliongeza kuwa wahamiaji hao haramu walikuwa kwenye gari dogo aina ya Hiace
lenye namba za usajili T 287 ASK ambayo ilikuwa imekodiwa na watu hao.
Gari hilo lilikuwa likiendeshwa
na dreva Edward John(27)mkazi wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambapo
wahamiaji hao haramu walikuwa wanatokea Nzega kwenda jijini Dar es salaam.
Baada
ya kuhojiwa na polisi walidai kuwa ni familia moja ambapo katika safari hiyo
walikuwa wakiongozwa na mwenyeji wao Bi.Anna Gigwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilaya ya Igunga Bw.Abeid Maige aliwataja majina wahamiaji hao kuwa ni Gaudensia January(22)mkazi wa Mwenge jijini Dar es salaam, Benard
Simon(43)mkazi wa Bagamoyo.
Alisema kuwa wengine ni Uwezo
Rwanzila(30)mkazi wa Dar es salaam,Meshack Asher(19)mkazi wa Dar es
salaam,Mwamvua Saidi(28)mkazi wa Kibondo,Modester Rwanzima(23)mkazi wa Dar es
salaam.
Wengine ni Shadrack Jonasi(23)mkazi wa Dar es
salaam,Samwel January(25)mkazi wa Ussoke Tabora pamoja na Amoni
January(27)mkazi wa Dar es salaam.
Alisema kuwa
watu hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi na kuongeza kuwa wamefanya
mawasiliano na Ofisi ya uhamiaji iliyoko Nzega ili waweze kuja Igunga kwa ajili
ya mahojiano zaidi.
No comments:
Post a Comment