Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya push Push Media Mobile Rugambo Rodney |
Mwandishi
Wetu
Kampuni ya
Push Mobile Media itatoa zawadi ya gari aina ya vits kwa mshindi wa promosheni
ya tamasha la Fiesta litakalofanyika mkoani Mwanza ijumaa hii.
Meneja
Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa watatoa gari
aina ya Vitz kwa mpenzi wa Fiesta atakayeshiriki katika tamasha hilo kwa kutuma
neon Fiesta kwenda namba 15678 na kuigingia katika bahati nasibu hiyo.
Rodney
alisema kuwa mbali ya kushinda gari, mshiriki pia anaweza kushinda fedha
taslimu kiasi cha shs 100,000 kwa siku. Pia mpenzi wa Fiesta anaweza kushinda
pikipiki.
Mshindi wa
mkoa wa Mwanza atakuwa wa pili kupata gari ambapo mshindi wa kwanza wa gari
alikuwa Abdallah Ally Ngagari (51) aliyeshinda kupitia tamasha la fiesta la
Kigoma.
“Tumepania kutoa zawadi katika mikoa yote
ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga zaidi ya sh milioni 80 ili kufanikisha
zoezi hili ambapo magari aina ya vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki,
tunawaomba mashabiki kushiriki kwa nguvu
zote,” alisema Rodney.
Wakati huo
huo; mkazi wa Shinyanga Rose Mahenda amafanikiwa kushinda pikipiki baada ya
kushiriki katika bahati nasibu hiyo.
No comments:
Post a Comment