THE UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Ijumaa, Septemba 13, 2013 amepokea hati za utambulisho za Balozi mpya wa Italia
katika Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Luigi Scotto.
Katika
halfa fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete ameishukuru Italia
kwa misaada ambayo nchi hiyo imekuwa inatoa kuchangia maendeleo ya Tanzania
ikiwamo kugharimia ujenzi wa Barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo.
Aidha,
Rais Kikwete amemtaka Balozi huyo mpya kuisaidia kuyashawishi makampuni zaidi
ya italia kuja kuwekeza katika uchumi wa Tanzania. “Tumekuwa na makampuni makubwa ya
Italia yaliyopata kuwekeza katika uchumi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na Agip na
Incar lakini bado tunahitaji uwekezaji zaidi ili tuweze kuimarisha zaidi uchumi
wetu,” Rais Kikwete amemwambia Dkt. Scotto.
Naye
Balozi huyo mpya amesema kuwa amefurahi sana kuteuliwa kuwa Balozi katika
Tanzania. “Ndoto yangu kubwa tokea nikiwa mtoto ilikuwa ni kufanya kazi katika
nchi iliyomtoa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere”.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM.
13
Septemba, 2013
No comments:
Post a Comment