Na Bbc Swahili
Wataalamu wa kuchunguza mauaji kutoka nchini Marekani
na Uingereza wamejiunga na kikosi cha wataalamu nchini Kenya kudadisi
hali katika jengo la Westgate.
Akiwahutubia waandishi wa habari katika eneo la shambulizi, Ole Lenku alisema kuwa jumba la West Gate limekabidhiwa kwa wakuu wa ujasusi kwa shughuli zaidi za udadisi.
Aliongeza kuwa idadi ya maiti walio ndani ya jengo hilo chini ya vifusi , haijulikani ingawa alisisita kama bado kuna maiti idadi yao ni ndogo sana.
Maafisa wataendesha shughuli ya kuondoa vifusi ili kuondoa miili iliyonaswa katika jengo hilo.
Jengo la Westgate lilitekwa na magaidi Jumamosi mchana huku wakiwaua watu kiholela na kuwateka baadhi.
Takriban watu 61 waliuawa na magaidi hao wakiwemo maafisa sita wa usalama huku washukiwa wengine 11 wakikamatwa.
Rais Kenyatta alifanya mkutano maalum na baraza la mawaziri kuhusu shambulizi hilo ili kudadisi hali itakayofuata.
No comments:
Post a Comment