Na Mwandishi wetu
Watanzania
sasa wanaweza kupata taarifa mbali mbali zikiwa pamoja na za michezo,
burudani kupitia simu ya mkononi baada ya kampuni ya Push Mobile Media
kutambulisha huduma mpya ya simu tv.
Meneja
wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Push Media Mobile, Rugambo Rodney
alisema kuwa ili kuweza kupata huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno SIMUTV
kwenda namba 15678 na kufuata maelekezo ili kupata huduma hizo ambayo
pia inapatikana kwa kupitia njia ya mtandao www.simu.tv.
“Tumeamua
kuanzisha huduma hii ili kuwawezesha watanzania kupata taarifa mbali
mbali mbali moto moto kwa njia ya urahisi zaidi kupitia simu zao za
kiganjani,” alisema Rugambo.
Rugambo
alifafanua kuwa mbali ya huduma za michezo na burudani, pia watanzania
wanaweza kupata taarifa nyingine kama nyimbo za Qaswida, nyimbo za
injili, filamu, siasa, uchumi, Taarifa za habari, nyimbo mbali mbali kwa
njia ya video na biashara kwa kupitia simu zao za mikononi.
Alisema
kuwa huduma hiyo ni ya kwanza hapa nchini na pia inawawezesha watumiaji
kuona vipindi mbali mbali vinavyorushwa na vituo vyote vya televisheni
zote hapa nchini na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment