TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 4 October 2013

Swahili Fashion inatafuta vipaji vipya Afrika Mashariki


Katika mwaka was sita, Swahili Fashion Week inatafuta tena vipaji vipya  vya ubunifu kutoka Afrika Mashariki. Wabunifu katika tasnia ya mitindo watapata nafasi za kukuza ndoto zao za kuwa wabunifu wakuu katika tasnia hii. 

Shindano hili huchukua nafasi mara moja kwa kila mwaka chini ya maonyesho makubwa ya mitindo Afrika Mashariki ( Swahili Fashion Week)

 
“ Kama miaka iliyopita Swahili Fashion week inatoa tena mfumo kwa ajili wabunifu wanaochipukia kuonyesha uwezo wao wa hali ya juju kupitia mashindano haya ili kujenga tasnia mpya ya vipaji” Amesema Mratibu wa Mitindo Bw. Honest Arroyal
 
“Ilinijengea uzoefu mzuri kushiriki katika mashindano hayo mwaka jana, Asante sana kwa Swahili Fashion Week kwa kubadilisha maisha yangu “ John Kapatala, Mshiriki  wa shindano la wabunifu wanaochipukia 2012
 
Ukiwa ni mwaka wa 6 wa Swahili Fashion Week, Mpango wa kamati hiyo mwaka huu dhima (theme) ya shindano hili ni “Evolution” , dhima hiyo inawataka wabunifu chipukizi hao kubuni mavazi yanayoashiria mabadiliko, si lazima upya, ila yenye muonekano wa kitofauti na mzuri
 
“ Mwaka huu tunahitaji ubunifu uwe wa hali ya juu, tunahitaji kuona mabadiliko, na nikisema mabadiliko namaanisha maendeleo, tofauti na tunayoona kila siku, tunataka kuona muonekano wa kipekee ambao utaonyesha tofauti  kabisa na tunayoona kila mwaka” Washington Benbella, Meneja wa Swahili Fashion Week
 
Mashindano haya yasiyokuwa na kipingamizi cha umri  ni wazi kwa kila anaeamini ana uwezo wa kuwa mbunifu wa mitindo. “ Swahili Fashion week ni jukwaa mahususi kwa mbunifu kuonyesha kazi yake , na mashindano ya wabunifu chipukizi ni hatua ya kuanza fani”. Akisisitiza Benbella
 
Shindano lipo wazi kwa watu wote kutoka Afrika Mashariki na fomu za kujiunga zinapatikana kwenye tovuti  ya Swahil Fashion Week www.swahilifashionweek.com , na ofisi za BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania ), Ilala Sharif Shamba. Mwisho wa kujiunga ni tarehe 21, Octoba 2013


No comments:

Post a Comment