Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27 imeanguka baada ya
kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja
wa ndege mjini Lagos.
Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani nchini humo.
Ndega hiyo iliruka mwendo wa saa mbili unusu kutoka katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Murtala Mohammed.
Maafisa walisema kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na bomba la mafuta katika uwanja huo.
Haijulikani ikiwa mafuta hayo ndiyo yalisababisha ndege kulipuka.
Shahidi mmoja alimbia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na moshi mkubwa ukifuka kutoka katika sehemu ya ajali hiyo.
Maafisa wa usalama waliharakisha kwenda katika eneo la ajali na kuanza kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo
Chanzo:Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment