Polisi katika eneo la Mtwara Kusini mwa Tanzania
wamewazuilia watu wanaoshukiwa kuhudhuria mafunzo ya kundi la kigaidi la
Al - Shaabab.
Washukiwa pia walikuwa na silaha zilizokuwa zimetengezwa kienyeji tu.
Zaidi ya hayo, kamanda huyo wa polisi alisema walipokea taarifa za wananachi wiki moja iliyopita, kuhusu kundi hilo ambalo lilikuwa linapata mafunzo msituni.
Polisi wangali wanawahoji washukiwa hao wakitaka kujua miongoni mwa mambo mengine wadhamini na wafadhili wao.
Kamanda wa polisi alimtaja kiongozi wa kundi hilo kuwa Mohammed Makande mwenye umri wa miaka 39.
Kwa mujibu wa polisi, washukiwa watafikishwa mahakamani mara baada tu ya uchunguzi kukamilika.
Kumakatwa kwao kunakuja wakati ambapo visa vya ugaidi vimeongezeka katika kanda ya Afrika Mashariki hususan nchini Kenya na Somalia.
Wiki jana Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, aliwataka wananchi kuchukua hatua zaidi huku serikali ikidhibiti hali ya usalama katika maeneo yaliyo katika hatari ya kushambuliwa.
Chanzo:Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment