Uwanja wa klabu ya AC Milan wa San Siro umefungwa kwa
mashabiki kwa mechi ijayo kama adhabu kwa matusi walioangua wakati wa
mechi hapo jana.
Kwingine Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michezl Platini amesema kua mchezo huo unafaa kuongoza juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi katika michezo.
Kiongozi huyo aliyasema hayo kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa FIFA kutoka Afrika kusini Tokyo Sexwale amesema kwenye mkutano huo unaojadili ubaguzi wa rangi na mchezo wa mpira kwamba utandawazi wa vipimo vya ubaguzi wa rangi ni muhimu katika juhudi zake kupambana na ubaguzi wa rangi.
Mwanaharakati huyo wa ANC amesema kua FIFA ina mipango ya kuandaa mkutano wa kilele juu ya ubaguzi wa rangi kwa ushirikiano na Wkfu wa Mandela mapema mwaka ujao.''
FIFA litatoa maelezo zaidi kuhusu mpango wake wa kupambana na ubaguzi rangi kwenye mkutano wake huko Qatar mwezi Disemba.
Chanzo:Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment