Na Bbc Swahili
Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini Hayati
Nelson Mandela amezikwa katika kijiji cha Qunu mkoa wa Cape Mashariki
nchini Afrika Kusini.
Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi hayo.
Kiongozi mmoja wa kitaduni aliita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa. Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela wa Thembu.
Viongozi wa Afrika, familia na marafiki walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Nelson Mandela katika mazishi yake ya kitaifa katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela alikuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini.
Rais Jacob Zuma alisema kuwa safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha lakini raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na urithi wake.
Mandela alifariki tarehe 5 mwezi Disemba akiwa na umri wa miaka 95.
Siku ya kumi na ya mwisho ya maombolezi kufuatia kifo cha Mandela, imekamilishwa na Mandela kupigiwa mizinga 19 na jeshi huku mwili wake ukizikwa katika kijiji cha Qunu. Mishumaa 95 iliwashwa kila mmoja ikiwa ishara ya miaka ya Mndela
No comments:
Post a Comment