Na Mwandishi wetu
Igunga.
Watu sita wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi wamevamia maduka ya wafanyabiashara katika kijiji cha Ziba
kata ya Ziba wilaya ya Igunga mkoani Tabora na kufanikiwa kupora fedha.
Majambazi hao ambao
walikuwa na silaha zinazosadikiwa kuwa ni bunduki aina ya shortguni walivamia kijijini
hapo na kuanza kufyatua risasi hewani.
Kwa mujibu wa jeshi la
polisi wilaya ya Igunga lilisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa
3:30 usiku katika kata ya Ziba wilayani Igunga ambapo majambazi hao walivamia
maduka ya wafanyabiashara hao.
Aidha majambazi hao baada
ya kuanza kufyatua risasi hizo walimfyatulia
risasi katika mguu wa kushoto na kumjeruhi mfanyabiashara Malanda Issa(50)mkazi
wa Ziba na kumpora fedha kiasi cha shilingi mill 1.5.
Askali polisi kutoka wilayani
Igunga baada ya kufika katika eneo la
tukio walianza kupambana na majambazi
hao kwa kurushiana risasi ambapo walimfyatulia risasi mgongoni jambazi mmoja na
kufanikiwa kumuua.
Baada ya jambazi huyo
mmoja kufyatuliwa risasi na askali polisi na kuuliwa majambazi wengine walifanikiwa
kukimbia na kutokomea kusikojulikana.
Baadhi ya wananchi wa
wilaya ya Igunga wamelipongeza jeshi la polisi kwa kupambana na majambazi hao
na kufanikiwa kuuwa jambazi huyo mmoja.
Wananchi hao walisema kuwa
kuuawa kwa jambazi huyo ni fundisho kwa
majambazi wengine na kusema itasaidia kupunguza matukio ya ujambazi na utekaji
wa mabasi katika wilaya ya Igunga ambao umekuwa ukiwatesa wananchi hao mara kwa
mara.
Kwa upande wake kamanda wa
polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi Peter Ouma alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwasaka majambazi hao
waliokimbia.
Kamanda Ouma aliwataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kuwakamata majambazi
hao na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment