Mfalme Bhumibol Adulyadej wa Thailand amewataka
wananchi wa nchi hiyo kushikamana kwa manufaa ya nchi hiyo, katika
hotuba yake kwa taifa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Mapema wiki hii kulikuwa na mapigano makali kati ya polisi na waandamanaji.
Waandamanaji ambao wamekuwa wakitaka serikali ijiuzulu, walianza kuandamana tarehe 24 Novemba mwaka huu.
Walikubali kuacha kushambulia majengo ya serikali ili kupisha sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa mfalme wa nchi hiyo, lakini wakisema wataendelea na maandamano yao baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
Wananchi wa Thailand ambao wanamheshimu sana Mfalme King Bhumibol Adulyadej, ambaye kwa sasa anaishi katika eneo la Hua Hin.
Watu walijitokeza katika mitaa kumtakia heri mfalme wakati huu wa ghasia nchini humo.
Alhamisi, maelfu ya watu walielekea katika mji wa Hua Hin, karibu na makaazi ya mfalme ya Klai Kangwon, kwa matumaini ya kumwona.
Source:Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment