MWENYEKITI
CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU
WA CHADEMA MKOA
S.L.P
260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua
kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa
kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli
ndani ya chama.
Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa
kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa,
hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa
sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza
Maamuzi na vitendo vinavyoendelea ndani
ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa demokrasia ya kweli
tunayoihubiri mbele ya umma.
Kwa barua hii basi, nimeonelea bora
upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na dhamira yangu
inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.
Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza
mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu
tayari.
Ninatanguliza shukrani zangu za dhati
kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati kuu ya chama.
Kusimamia haki, katiba na misingi ya
chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba
macho pindi ujinga wa namna hii unapoendelea kutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.
Nakutakia kila la heri kwenye majukumu
yako.
………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu
No comments:
Post a Comment