Katika hotuba yake ya maneno 14,112 iliyosomwa kwa
saa 3:34, Jaji Warioba aliweka wazi maoni ya wananchi yaliyomo katika
ibara 271 za Rasimu hiyo, ukiwamo muundo wa Muungano wa Serikali Tatu –
Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.
Mwanasheria huyo alijenga hoja zake zilizoisaidia
Tume yake kufikia hitimisho la muundo huo, kwamba ilizingatia maoni ya
wananchi, yakiwamo ya mabaraza ya katiba ya Ofisi ya Makamu wa Rais,
Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambayo ama moja
kwa moja au kwa tafsiri yalipendekeza muundo wa Serikali Tatu.
Alisema tume hiyo ililazimika kupendekeza muundo huo kutokana na kero, hoja na malalamiko yaliyotolewa na pande mbili za Muungano wakati tume hiyo ikukusanya maoni, pamoja na hoja zilizotolewa miaka ya nyuma na tume mbalimbali.
Alisema tume hiyo ililazimika kupendekeza muundo huo kutokana na kero, hoja na malalamiko yaliyotolewa na pande mbili za Muungano wakati tume hiyo ikukusanya maoni, pamoja na hoja zilizotolewa miaka ya nyuma na tume mbalimbali.
“Suala la muundo wa Serikali Tatu limechukua
nafasi kubwa katika mjadala tangu tume ilipozindua Rasimu ya Kwanza ya
Katiba. Mjadala wa muundo wa muungano umekuwa mkubwa kiasi cha kufunika
mapendekezo mengine yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano,” alisema Warioba katika hotuba yake ya aya 191 ambayo
imechapwa kwa ukamilifu ndani ya gazeti hili.
Huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe, Jaji
Warioba alisema kwa tahmini ya tume hiyo, muundo wa Serikali mbili
hauwezi kubaki kwa hali ya sasa.
“Muungano wa Serikali mbili waliotuachia waasisi
siyo uliopo sasa. Umebadilishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya
kufanya mabadiliko kwenye Katiba. Waasisi walituachia Muungano wa nchi
moja yenye Serikali mbili na siyo nchi mbili zenye Serikali mbili,”
alisema.
Alisema muundo wa Serikali mbili unaweza kubaki tu
ikiwa orodha ya mambo ya muungano haitapunguzwa bali itaongezwa na
isipokuwa hivyo Serikali ya Muungano itabaki na rasilimali na mambo ya
Tanzania Bara tu.
“Katika hali hiyo, pande zote mbili zitaendelea
kulalamika. Kwa upande mmoja, Zanzibar itaendelea kulalamika kwamba
Tanzania Bara imevaa koti la Muungano kwa faida yake na kwa upande
mwingine, Tanzania Bara itaendelea kulalamika kwamba mambo yasiyo ya
Muungano ya Tanzania Bara na rasilimali zake, ndizo zimekuwa Muungano,”
alisema.
Warioba alishangiliwa tena na baadhi ya wajumbe
aliposema: “Muundo wa Serikali Tatu haupunguzi uimara wa Muungano na
muungano huo ni wa nchi mbili kwa manufaa ya wananchi, “Faida kubwa
iliyopatikana katika miaka hamsini iliyopita ni kuungana kwa wananchi.”
No comments:
Post a Comment