Baadhi ya wananchi wa Namanyere wilayani Nkasi wakichangia damu katika
siku ya uzinduzi wa siku ya Utepe mweupe.
MTANDAO wa Utepe Mweupe na Uzazi Salama (White Ribbon
Allience for Safe Motherhood) umekemea vikali tabia zinazofanywa na baadhi ya
watumishi wa hospitali na vituo vya afya ya kuuza damu ambayo kimsingi
inatakiwa kutolewa bure kwa wahitaji.
Kauli hiyo ya pamoja imetolewa jana
wilayani Nkasi na wanaharakati wa mtandao huo walipokuwa katika hafla ya
uzinduzi wa wiki ya Utepe Mweupe wilayani hapa, mkoani Rukwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo,
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ‘Evidence for Action’ ambao wanatekeleza mradi
ujulikanao kama ‘Mama Ye’, Craig John, alisema wamepata malalamiko toka kwa
wananchi ya kuwa kuna tabia ya baadhi ya watendaji kwenye sehemu za kutolea
huduma za afya huwauzia wagonjwa damu kitu ambacho hakikubaliki.
“...Wakati tunapita pita mitaani
kuhamasisha wananchi kuja kujitolea damu kwa ajili ya akinamama wajawazito
wanaohitaji kuongezewa damu, wananchi walituambia kuwa baadhi ya watendaji wa
afya wamekuwa kero kwao kwani wanawauzia damu pindi wanapokuwa wanaihitaji,”
alisema Craig.
Naye Mratibu wa Utepe Mweupe nchini,
Bi. Rose Mlay aliitaka serikali kutenga bajeti mahususi katika mwaka wa fedha
2014/2015 ili kuhakikisha vituo vya afya wanatoa huduma za dharura ikiwemo
upasuaji na damu salama.
“.Kama mtoto amekaa vibaya tumboni kwa
mama au hata kama amepigwa mwanamke huyu anaweza kusaidiwa kwa kufanyiwa
upasuaji na kuongezewa damu salama pekee, hivi ndivyo vitakavyo muokoa,”
alisema Rose.
|
No comments:
Post a Comment