Timu ya taifa ya Tanzania kwa
watoto wa mitaani imenyakua Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani, katika
mashindano yaliyozishirikisha timu za mataifa mbalimbali duniani huko
Rio de Janeiro, Brazil hapo jana.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Tanzania ilikuwa ikiongoza kwa magoli 2-0. Kipindi cha pili iliongeza bao la tatu. Burundi iliweza kupata bao la kufutia machozi zikiwa zimebakia dakika nne mpira kumalizika.
Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuonyesha kiwango cha juu hata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino na Argentina.
Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano hii ya kombe la dunia.
Hii ilikuwa mara ya Pili kwa timu ya Tanzania kutinga fainali za michuano hiyo ya dunia kwa watoto wa mitaani inayofanyika siku chache kabla ya fainali za Kombe la Dunia kuanza mwezi Juni.
Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za michuano hii kule Durban Afrika Kusini mwaka 2010 Tanzania ilifungwa na India katika fainali.
Mashindano haya hutambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA
Chanzo.BBC Swahili
Mwisho.
No comments:
Post a Comment