Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ametangaza wazi kuudhika sana na safu yake butu ya mashambulizi.
Mourinho aliyasema hayo punde baada ya kushuhudia PSG ya Ufaransa ikiititima 'the blues' mabao matatu kwa moja katika mkondo wa kwanza wa mechi ya robo fainali ya kombe la mabingwa Barani Ulaya.
Vijana wa Jose Mourinho nao wakajifurukuta na kufanya mashambulizi ambayo yalizaa penalti baada ya Oscar kuchezewa visivyo katika eneo la lango.
Eden Hazard akafanya mambo kuwa 1-1 katika dakika ya 27.
Nipe nikupe iliendelea hadi kipindi cha pili PSG walipofaidika na bao la kujifunga mwenyewe la David Luiz kunako dakika ya 61.
Hawakukomea hapo ,Javier Pastore alihakikisha Chelsea itakuwa na mlima wa kupanda nyumbani kwao Stamford Bridge katika mkondo wa pili mbali na kuibua kumbukumbu za mwaka wa 2004 timu hizo mbili ziliposajili matokeo sawia na hayo PSG ilipokuwa mbioni kucheza katika fainali ya kombe la mabingwa .
Aidha mechi ya kwanza kwa mkufunzi Jose Mourinho alipochukua hatamu Stamford bridge ilikuwa dhidi ya Paris St-Germain mwezi September 2004.
Wakati huo The Blues waliwatandika PSG 3-0 John Terry na Didier Drogba wakiandikisha majina yao katika orodha ya wafungaji.
Chanzo:Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment