TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 2 June 2014

Justin Bieber aomba radhi kwa ubaguzi

Bbc Swahili

Justin Bieber

Mwanamuziki maarufu duniani Justin Bieber, ameoamba radhi kwa kutumia neno la kibaguzi wakati akiwakejeli wamarekani weusi kuhusu swala la ubaguzi wa rangi.

Bieber alitumia neno hilo N***** katika kikao na marafiki zake alipokuwa anafanya vichekesho kuhusu swala la ubaguzi wa rangi.

Kanda ya video ya Bieber akitamka neno hilo, iliwekwa kwenye mtandao wa The Sun Jumapili.
Jarida hilo linadai kuwa marafiki za Bieber wamekuwa na ufahamu kuhusu kanda hiyo na wamekuwa wakitumia pesa kujaribu kuificha.

Katika kanda hiyo Bieber anasikika akiuliza kwa nini wamarekani weusi wanaogopa misumeno inayotumia nishati.

Kanda hiyo inamalizika kwa Bieber kukejeli wamarekani wausi kwa kutoa sauti ya msumeno na kisha kurejelea kauli hiyo ya ''Kimbia N*****'' mara tano.

Hata hivyo inasemekana kanda hiyo ilirekodiwa kama sehemu ya makala maalum kumhusu msanii huyo.
Justin Baieber na mwanamasumbwi Floyd Mayweather

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 20, ametoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema: '' Naomba radhi kwa yeyote aliyehisi kukerwa na matamshi yangu.''

Mapema jumatatu mwanamasumbwi, Floyd Mayweather, aliweka picha hii kwenye mtandao akiwa na Bierber kama ishara ya kumuunga mkono.

"Justin amekuwa mzuri sana kwangu na familia yangu. Sote ni binadamu na hufanya makosa , ni sehemu tu ya kuelekea katika utu uzima. Nina furaha kwa kile anachokifanya kama mwanamuziki na mfanyabiashara,"

No comments:

Post a Comment