Mexico walipata pointi moja
dhidi ya Brazili, katika mechi ya kundi A iliyomalizika bila ya timu
yeyote kutikisa wavu wa mwenziye katika uwanja wa Estadio Castelao huko
Fortaleza.
Fred alipatikana kuotea kwenye lango mara tatu mfululizo.
Licha ya Mashambulizi ya Neymar ,kipa wa mexico Ochoa alihakikisha mechi hiyo inaisha sare tasa.
Ochoa tena aliokoa jaribio lingine la Neymar katika kinyang’anyiro katika lango la Mexico. Jaribio lingine la Jo lilizuiwa na Ochoa; kipa wa Mexico.
Kisha mpira wake Silva, kwa kichwa, kutoka kwa kona yake Neymar, ukasimamishwa tena na Ochoa katika dakika ya 85.
Wito wa Brazili wapewe penalti Marcelo alipoanguka kwa urahisi mbele ya lango la Mexico uliambulia patupu.
Mexico kwa upande wao hawakuwa na nafasi nyingi, ila wakati ule Hector Herrera alipiga mkwaju uliopita kidogo juu ya lango la Brazil.
Matokeo haya yanaziwacha timu zote mbili zikiwa na alama nne katika kundi lao, zikiwa zimesalia na mchuano mmoja kucheza.
No comments:
Post a Comment