TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Saturday, 26 September 2015

Kikosi cha kumlinda rais chavunjwa Burkina Faso


 

Bbc Swahili
Serikali ya Burkina Faso imevunja kikosa cha kumlinda rais ambacho kiliwashika mateka mawaziri wakati wa majaribio ya mapinduzi yaliyofeli.

Hatua hiyo ilichukuliwa wakati wa mkutano wa kwanza wa serikali tangu siku ya jana  wakati rais wa mpito Michel Kafando aliporejeea madarakani.

Waziri wa masuala ya ulinzi amefutwa kazi na tume imebuniwa kuwatambua wale waliohusika katika kupanga mapinduzi hayo.
Takriban watu 19 waliuawa wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi hayo.

No comments:

Post a Comment