Sherehe za utoaji tuzo kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwa miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete sasa zitafanyika Oktoba 12 badala ya tarehe iliyotangazwa awali.
Taswa licha ya kutoa tuzo kwa wachezaji
waliofanya vizuri zaidi, pia itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake katika michezo wakati
wa uongozi wake.
Baadhi
ya mambo hayo ni serikali yake ilivyolipia makocha wa michezo ya soka, netiboli na ngumi
na pia serikali ilipeleka wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa
maandalizi ya mashindano ya kimataifa.
Pia serikali yake ilirejesha michezo shuleni
pamoja na mashindano ya michezo kwa shule za msingi na sekondari (UMITASHUMTA
na UMISETA).
Pia tukio hilo la tuzo itakuwa sehemu ya
wanamichezo kumuaga Rais Kikwete ambaye anamaliza muda wake kikatiba baada ya
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Maandalizi muhimu kwa tukio hilo yamekamilika
ikiwa ni pamoja na kupata majina ya wanamichezo hao watakaopewa tuzo siku hiyo.
Alhamisi wiki hii Taswa itatangaza wadhamini
wengine watakaoungana na wadhamini ambao tayari wametangazwa ambao ni GSM
Foundation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Ahsnateni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
05/10/201
No comments:
Post a Comment