BBC SWAHILI
Kakaake mkubwa nyota wa timu ya Argentina na Barcelona Lionel Messi amekamatwa kwa kumiliki bunduki bila kibali.
Polisi wanasema kuwa Matias mwenye umri wa miaka 33 alikataa kuonyesha vibali vyake aliposimamishwa katika mji wa Rosario.
Polisi walilikagua gari lake na kupata bunduki ambayo Matias ameshindwa kutoa kibali chake cha umiliki.
Maafisa hao wanasema kulikuwa na mvutano kati yao na ndugu huyo wa Messi ambapo alijeruhiwa katika jicho huku maafisa hao wakipata majeraha madogo.
Baadaye alipelekwa katika kituo kimoja cha polisi mjini Rosario na kuzuiliwa kwa kwa saa nne.
Alikamatwa mara moja kabla ya mwaka 2008 kwa kubeba silaha bila kibali.
Watu wa familia ya Messi pia wanakabiliwa na madai ya kukwepa kulipa kodi nchini Uhispania.
Lionel Messi na babaake Jorge wote wanatuhumiwa kuiibia mamlaka zaidi ya yuro milioni 4 zinazohusishwa na mapato kutokana na matumizi ya jina lake.
No comments:
Post a Comment