TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 16 December 2015

Contest for cartoons on international affairs open [Worldwide]

 IJNET
Cartoonists who focus on international affairs can submit their work to this contest.

The Overseas Press Club of America is accepting applications for its Thomas Nast Award for best cartoon on international affairs. This year the contest is open to non-English entries.

Works must have been published or broadcast in the United States or by a U.S.-based company or be accessible to an American audience in 2015. An English translation must be provided for cartoons about international events not published originally in English.
 
The deadline is Jan. 29, 2016. The entry fee is US$200.
For more information, click here.

NYU offers journalism fellowship [Worldwide]

 IJNET
Journalists with at least two years of experience and fluency in English and at least one other language can apply for a fellowship in New York. 

The Arthur L. Carter Journalism Institute at New York University (NYU) is seeking applications for the World Journalist Fellowship.

The fellowship provides international journalists with two semesters of funding to study at one of the master’s programs at the Arthur L. Carter Journalism Institute, as well as a US$13,000 stipend.

Fellows can choose one of 10 concentrations: business and economic reporting; cultural reporting and criticism; global and joint program studies; literary reportage; magazine writing; news and documentary; reporting New York; reporting the nation; science, health and environmental reporting; and Studio 20.

Candidates must also complete the application for the graduate program of their choice. The GRE and TOEFL are required tests for admission to NYU.

The deadline is Jan. 4, 2016.

For more information, click here.

Monday, 30 November 2015

Kili Stars yatolewa Chalenji

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa  Kilimanjaro Stars imetolewa katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 dhidi ya wenyeji Ethiopia baada ya  kucheza dakika 90 na kupata  sare ya bao 1-1.
 
Katika mchezo huo wa Robo Fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Kili Stars iliongoza kwa bao lililofungwa  na  John Raphael Bocco ‘Adebayor’ baada ya kupata pasi ya Deus Kaseke dakika ya 25.

 
Ethiopia walisawazisha kipindi cha pili dk. 57 katika bao lililofungwa na  Panom Gathouch baada ya Mohammed Naser kuangushwa na  Shomary Kapombe

Waliokosa penalti ni Shomary Kapombe na  Jonas Mkude huku waliofunga ni Himid Mao, mshambuliaji Bocco na beki Hassan Kessy.

 
Waliofunga penalti za Ethiopia ni Panon Gathouch, Mohammed Naser, Ashalew Tamene na Behaylu Girima.  

 
Aidha,  Uganda imeifunga 2-0 Malawi mabao ya Farouk Miya na Ceasar Okhuti na sasa itakutana na Ethiopia katika Nusu Fainali.

U 15 yakabidhiwa bendera

Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) jana ilikabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.

Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel aliwashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.

Ole Gabriel amewataka vijana waliochaguiwa katika kikosi hicho, kuitumia nafasi hiyo adimu ipasavyo kuwawakilisha watanzania, kujituma katika mafunzo wanayopewa na waalimu wao, nidhamu ndani na nje ya uwanja na kuonyesha uzalendo wao wanapoiperesuha bendera ya Taifa.

Kikosi hicho cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 kinatarajiwa kuondoka kesho alfajiri (Jumatatu) kuelekea jijini Mwanza kwa mchezo wa kirafiki na kombaini ya mkoa wa Mwanza (U17), kisha kuelekea mkoani Kigoma kwa michezo miwili ya kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).

Baada ya michezo ya mkoani Kigoma, U15 itaelekea Kigali Rwanda kwa michezo na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, kisha Jinja kucheza na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Uganda, Nairobi itacheza na timu ya taifa ya Kenya (U17) na kumalizia jijini Arusha kwa kucheza na kombaini ya mkoa wa huo (U17).

Timu inatarajiwa kurejea jijini Dar ess alaam Disemba 24 baada ya kuwa imecheza michezo kumi ya kirafiki, mechi hizo zitampataia nafasi kocha mkuu Sebastiani Mkomwa kuona maendeleo ya vijana wake, wakiajiandaa kucheza michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika U17 mwaka 2017 nchini Madagascar.

 
 

Michuano ya Mitumbwi Mwanza yaiva

Meneja Mauzo na Usambazaji waKampuniya Bia Tanzania (TBL) Kanda yaZiwa, Godwin Zakaria (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha MitumbwikandayaZiwa, Richard Mgabo, moja ya vikombe vitakavyoshindaniwa katika mashindano ya  mbio za Mitumbwi  wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Mwanza mwishonimwa wiki kwa udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager

Mwenyekiti  wamitumbwi Kanda yaZiwa, Richard  Mgambo (katikati), akinyanyua juu moja ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda yaZiwa, Godwin Zakaria ( kulia) atakalokabidhiwa bingwa wa mbio za makasia mara baada ya uzinduzi wa mashindano hayo yaliyofanyika TBL Mwanza mwishoni mwa wiki kwa udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager. Wengine ni viongozi wa mikoa katika maeneo ambako fainali zitafanyika



Wednesday, 21 October 2015

Matokeo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

MATOKEO LIGI YA MABINGWA ULAYA JANA
FC Porto 2 - 0 Maccabi Tel Aviv
Dynamo Kyiv 0 - 0 Chelsea
Valencia CF 2 - 1 KAA Gent
Zenit St Petersburg 3 - 1 Lyon
Bayer 04 Leverkusen 4 - 4 Roma
BATE Borisov 0 - 2 Barcelona
Arsenal 2 - 0 FC Bayern Munchen
Dinamo Zagreb 0 - 1 Olympiakos

Tuesday, 20 October 2015

Yaya Toure kushindania tuzo kuu ya soka duniani

 BBC SWAHILI

Yaya Toure 

Wachezaji watatu wa Manchester City Sergio Aguero, Kevin De Bruyne na Yaya Toure ni miongoni wa wachezaji 23 walioorodheshwa kushindania tuzo ya Ballon d'Or.

Kiungo wa Chelsea Eden Hazard na mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez pia wamo kwenye orodha hiyo ya kuteua mchezaji bora wa mwaka duniani.

Tuzo hiyo ya Ballon d'Or kwa sasa inashikiliwa na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye pamoja na Lionel Messi wa Barcelona, wamekuwa wakishinda tuzo hiyo kwa miaka saba iliyopita. Wawili hao bado wamo kinyang’anyironi mwaka huu.

Mshambuliaji wa Real Madrid kutoka Wales Gareth Bale ndiye mchezaji Mwingereza pekee aliyetajwa kwenye orodha hiyo.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho na mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger nao wamo kwenye orodha ya wakufunzi 10 watakaopigania tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka.

Watamenyana na meneja wa Barcelona Luis Enrique na kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola.
Katika orodha hiyo, La Liga ya Uhispania inaongoza kwa kuwa na wachezaji 11, nayo Bundesliga ya Ujerumani ina wachezaji sita. Serie A ya Italia ina wachezaji wawili.

Ufaransa inawakilishwa na mchezaji mmoja pekee, kigogo wa Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic.

Raundi ya 11 ya Ligi Kuu kuchezwa Desemba 12

 
 Mechi za raundi ya 11 za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zichezwe Novemba 7 na 8 mwaka huu sasa zitafanyika Desemba 12 na 13 kupisha maandalizi ya Taifa Stars ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

Taifa Stars inatarajia kuingia kambini mapema mwezi ujao kujiandaa na mechi ya kwanza dhidi ya Algeria ambayo itafanyika Novemba 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana nchini Algeria, Novemba 17 mwaka huu.

Mechi hizo za Vodacom zitakazochezwa Desemba 12 ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga (Tanga), Kagera Sugar na Ndanda (Tabora), Stand United na Mwadui (Shinyanga), Mbeya City na Mtibwa Sugar (Mbeya), Azam na Simba (Dar es Salaam) na Majimaji na Toto Africans (Songea). Mechi za Desemba 13 ni kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons (Dar es Salaam), na Coastal Union na African Sports (Tanga).

Pia mechi tatu za raundi ya sita ambazo hazikuchezwa Oktoba 4 mwaka huu kupisha mechi ya Taifa Stars na Malawi sasa zitafanyika Desemba 16 mwaka huu. Mechi hizo ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar (Dar es Salaam), na African Sports na Yanga (Tanga), mchezo kati ya Ndanda na Simba (Mtwara utapangiwa tarehe ya kuchezwa.

Nayo mechi namba 59 kati ya JKT Ruvu na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Oktoba 21 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam imesogezwa mbele kwa siku moja hadi Oktoba 22 mwaka huu ili kuipa nafasi ya mapumziko JKT Ruvu ambayo jana (Oktoba 18 mwaka huu) ilicheza mechi yake ya raundi saba mkoani Shinyanga.

Ligi Kuu ya Vodacom kuendelea kesho

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti nchini, huku timu 8 zikisaka kupata pointi tatu muhimu.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Toto Africans, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni, mjini Shinyanga Stand United watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Kambarage mjini humo.

Tanzania Prisons watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Wagosi wa Kaya, Coastal Union wakiwakaribisha Kagera Sugar katika uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.

Alhamis ligi hiyo itanendelea kwa michezo minne pia kucheza katika viwanja mbalimbali, JKT Ruvu wataikaribisha Mtibwa Sugar uwanaj wa Karume jijini Dar es salaam, Mwadui FC watacheza dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.

Jijini Mbeya, Mbeya City watawakaribisha African Sports katika uwanja wa Sokoine, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa waoka mikate wa bakhresa Azam FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.


Kiiza mchezaji bora wa Septemba

Hamis Kiiza

Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Septemba. 

Kwa kuibuka mchezaji bora, Kiiza atazawadiwa sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.

Kiiza ambaye ameisadia Simba kufanya vizuri kwenye mwezi huo, ikiwemo kufunga mabao matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar aliwashinda washambuliaji wa timu za Stand United (Elias Maguli) na Yanga (Amisi Tambwe).

Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa raundi tano, Kiiza amefunga jumla ya mabao matano.

Monday, 19 October 2015

Fursa kwa waandishi wa habari

 IJNET

Experienced journalists with an innovative idea for addressing a particular journalism challenge can apply for a 10-month fellowship in California.

Each year, the John S. Knight Journalism Fellowships selects 20 fellows to spend an academic year at Stanford University. During their fellowship, they have access to some of the world’s most innovative thinkers and organizations, from technology giants to hot new startups to Stanford’s 100-plus special institutes and centers.

Fellows receive a stipend of US$65,000 as well as supplements for housing, childcare, health insurance and moving expenses. Tuition costs at Stanford are also covered.

Ideally, U.S. candidates will have at least seven years of experience, and international candidates should have at least five years of experience.

The deadline to apply is Dec. 1.

For more information, click here.

Fursa kwa waandishi wa habari hiyo

 IJNET

Students or recent graduates with a strong interest in journalism can apply for paid internships.
The Thomson Reuters Journalism Internship program is accepting applications for its 2016 summer cycle. Most internships are in its New York and Washington bureaus, but opportunities may also exist in Toronto, Mexico City and São Paulo, as well as our other U.S. offices.  Internships will last 10 weeks.

The programs are crash courses in business, political and general news reporting. Interns will receive several days of formal training before they start work. Every intern will report to a senior editor and be assigned a journalist mentor who will be available to provide advice and guidance.

Candidates must have completed at least two years of university, some prior journalism experience, excellent writing and communications skills.

The application deadline Dec. 1.

For more information, click here.

Kamati ya Taifa Stars yatambulishwa rasmi

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars Farough Baghozah (Katikati), Makamu wake Michael Wambura na Katibu Teddy Mapunda wakizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani)

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars iliyoteuliwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bwana Farough Baghozah leo hii amekutana na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuitambulisha rasmi kamati hiyo.

Katika kamati hiyo ya Taifa ya Stars wapo Michael Wambura – Makamu Mwenyekiti, Bi Teddy Mapunda – Katibu, Wakili Imani Madega – Mweka Hazina, na wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac Chanji, Salum Abdalla na Moses Katabaro.

Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kutangaza kamati ndogondogo na wajumbe wake kama ifuatavyo:

 1. Maandalizi ya timu, zikiwemo huduma kwa timu ya Taifa stars
 Mwenyekiti – Imani Madega
 Wajumbe – Msafiri Mgoyi,Teddy Mapunda.

2. Uhamasishaji wa mchezo (Michezo ijayo) na Masoko
 Mwenyekiti – Juma Pinto
 Wajumbe – Baraka Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim  Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon,  Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.

 3. Kamati ya Fedha
Mwenyekiti – Farough Baghozah
Wajumbe – Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega,          Juma Pinto,        Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.

4. Mikakati ya ushindi – itakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.

Pia kamati imetangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza kutumika kuanzia leo hii.  Pia Kamati imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.

Timu inatarajia kuweka kambi Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.

Aidha, Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa nyumbani.  Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa Kamati Bwana Farough Baghouzah.

Monday, 12 October 2015

Djokovic, Muruguza wababe China Open

 

 BBC SWAHILI
 Mcheza tenesi namba moja kwa ubora kwa upande wa wanaume Novak Djokovic ametwaa taji la michuano ya wazi ya China.

Djokovic alimshinda Rafael Nadal anayeshikilia nafasi ya nane kwa ubora wa mchezo huo duniani kwa
Seti 6-2 6-2 na kushinda taji lake la sita kwa mwaka huu.

Na kwa upande wa wanawake Muhispani Garbine Muguruza alipata ushindi wa seti 7-5 6-4 dhidi ya Timea Bacsinszky na kutwaa taji la pili.

Kwa ushindi huo Muguruza anapanda mapka nafasi ya nne kwa ubora wa viwango vya mchezo huo.

Madam Ritha atoa tamko kuhusu ushindi wa Kayumba




 Kufuatia malalamiko ya ushindi wa mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS) kwa mwaka huu Kayumba Juma, jaji mkuu wa shindano hilo Ritha Paulsena ametoa tamko.


Kayumba alishinda shindano hilo juzi ambapo alijinyakulia kitita cha Milioni 50 pamoja na mkataba wa kusimamiwa kazi zake za sanaa wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 10 kutoka Tip Top Connection.


Kayumba alishinda akiwa amemwacha mshindani mwenzake Nassib Fonabo ambae watu mbalimbali ndio wamekuwa wakilalamika kuwa ndie alietakiwa kuwa mshindi.


Akizungumzia sakata hilo Jaji Mkuu huyo alisema kuwa kwa kawaida kazi ya majaji inakuwa ni kuwachuja washiriki kutokea mikoani na hadi kufikia hatua ya tano bora ambapo kwa mwaka huu ilikuwa ni hatua ya sita bora kutokana na ushindani kuwa mkali zaidi.