Na Hafsa Golo
Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza
kuwa watu wawili za zaidi wameripotiwa kubakwa baada ya kuzungwa kimazingara na
kupandishwa juu ya varanda za nyumba za Michenzani na kufanyiwa unyama huo.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi ofisini kwake katika hospital ya Mnazi Mmoja, Dk. Msafiri Marijani alisema
kwamba watu wawili wameripoti hospitali kwa uchunguzi baada ya kufanyiwa
vitendo hivyo.
Alisema baada ya kuongezeka kwa
matukio hayo wameamua kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili liweze kufuatilia
kwa kina kuwepo kwa vitendo hivyo vinavyoendelea kujitokeza.
“Hali imekuwa si ya kawaida kwani
mbali na wanawake wa mwanzo waliofika hapa mwisho wa wiki, tumepokea wengine
wawili ambao wamekumbwa na tatizo hilo, hivyo kwa kushirikiana na wahusika
tumetoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa vile inawezekana ikawa hawana taarifa”,
alisema.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mjini Magharibi Azizi Juma Mohammed alithibitisha kupokea taarifa hizo
kutoka wizara ya afya na kueleza kuwa wahusika waliokumbwa na tatizo hilo ambao
baadhi yao wamefika katika kituo cha polisi Madema kuripoti.
Alisema kwa nyakati tofauti
wamepokea taarifa juu ya kutokea tatizo ambapo maeneo yanayotumika kwa
kufanyika vitendo hivyo ni juu varanda ya jumba namba tano ya Michenzani ambayo
imeonekana kuwa hakuna kidhibiti cha kuingia kama yalivyo nyumba kama hizo.
Alisema vijana hao hufika katika
maeneo hayo na kujitambulisha kuwa ni askari wa jeshi la polisi au polisi jamii
na hutumia njia ya kuwatisha na hata kuwabana kisheria kama wahusika
wanakabiliwa na shitaka huku wakiongozana nae na hatimae huwafikisha juu
varanda kwa kuwafanyia vitendo hivyo.
“Wanaokumbana na matokeo hayo baadhi
yao wale ambao hukaa faraha na wanaume aidha huwa mke wa watu, au mwanafunzi
kaaga kwao anaenda tushweni kwa kuogopa kujulikana ndipo anapoamua kuwafuata na
kukutana na matatizo hayo na wengine hukutikana njiani”, alisema
Aidha alisema mbali na kuwabaka pia
huwanyanganya mali zao ikiwema dhahabu, simu na pesa na hata kuwapiga na
kusababishia majeraha katika miili yao.
Mbali na hayo kamanda alisema kuwa
watajipanga kuanzisha mikakati madhubuti ya kupambana na matukio hayo ikiwemo
kuandaa operation katika maeneo yaliojitikeza vitendo hivyo na pia kuwatumia
askari wainteligensia.
Hivi karibuni waziri wa Ustawi wa
Jamii,Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, Zainab Omar, aliwataka wananchi
kuwa na mashirikiano ambayo yatasaidia kuondokana katika vitendo hivyo vya
udhalilishaji na ukatili.
Alisema kuwa vitendo vya ubakaji na
udhalilishaji vinawaathiri watoto na akina mama kiakili, kiafya na hata
kimwili,hivyo alisema kuwa ili jamii ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla
kunahitajika mashirikiano.
“Nakuombeni akina mama,akina baba na
wazazi wenzangu kwa ujumla tuwe na mashirikiano madhubuti ambayo yatasaidia
kuondosha hivi vitendo vya udhalilishaji ambavyo vinamuathiri mtoto na
mzazi,kiakili,kiafya na hata kimwili,”alisema.
Hivyo alifahamisha kuwa serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, haikubaliani na vitendo hivyo na kuahidi kwamba, serikali haikubaliani na vitendo hivyo na kuahidi kwamba,
serikali itachukuwa hatua kali katika kukabiliana na tatizo hilo ambalo
limekuwa liikabili jamii.
Kwa hisani ya Swahilivilla blog
No comments:
Post a Comment