R.I.P Mangwea |
KAMPUNI ya QS Mhonda J Entertainment imeandaa tamasha la kuibua warembo bora linalofahamika kama QS Queen utamu extra night likiwa na lengo la kuwapa mashabiki nafasi ya kuichangia familia ya marehemu Albert Mangwea aliyefariki hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa
habari Maelezo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Fred Felix alisema tamasha hilo
litafanyika Juni mosi katika ukumbi wa Dar Live Mbagala.
Felix
alisema awali, kabla ya kifo cha msanii huyo tayari kampuni hiyo ilikuwa imeshapanga kuwepo kwa tamasha hilo, hivyo
baada ya kutokea kwa matatizo hayo, imeona isihairishe na badala yake waendelea
na tamasha hilo kama ambavyo walipanga na fedha zitakazopatikana ziwe kama
rambi rambi kwa familia ya msanii huyo.
“Tunatoa
salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Albert Mangwea ambaye tunatambua
mchango wake katika tasnia ya muziki, baada ya kutafakari sana uongozi wa
kampuni ukaona itakuwa ni jambo jema kuendelea na tamasha ili kuwapa mashabiki
nafasi ya kuichangia familia yake,”alisema.
Alisema
kutakuwa na kipindi maalum siku hiyo ambako kila ambaye atafika atapata nafasi
ya kutoa rambi rambi zao na kuifikia familia ya marehemu kupitia kwa mwakilishi
wa familia hiyo.
Amewaomba
warembo mbalimbali wajitokeze siku hiyo na kutoa kiingilio cha sh. 10,000 ili waweze kujikatia tiketi ya ushiriki ,
ambapo miongoni mwa warembo watakaohudhuria
na kuonyesha vipaji vyao mbalimbali watachaguliwa walio bora zaidi kwa
ajili ya kukaa ndani ya nyumba moja na warembo wengine ambao watatafutwa katika
mikoa mingine.
Alisema
baada ya tamasha hilo wataenda katika mikoa ya Mwanza, Mtwara, Mbeya, Singida,
Dodoma, Kilimanjaro, Arusha na mikoa mingine kwa lengo la kutafuta warembo
wengine kisha kuwachanganya na wa Dar es Salaam watakaokaa jumba moja
litakaloitwa QS Queens utamu extra house.
Felix
alisema warembo hao watakaa kwa miezi
miwili huku wakiwa wanalipwa posho na
kupigiwa kura na wananchi kisha kutafuta mshindi wa jumla ambaye ataondoka na
gari na ajira ya kudumu ambayo ni kuwa Balozi wa Kampuni hiyo.
Baadhi ya
wanamuziki wakali kama Ney wa Mitego, Madee, Juma Nature, Inspector Haroun, Mb
Dog, Solid Ground Family, Hadija Kopa, Diamond na wengine kibao wataburudisha.
No comments:
Post a Comment