Waokoaji wakivunja bomba la maji taka kumuokoa kichanga huyo. |
Mtoto
mchanga aliyeokolewa kutoka bomba la kupitishia maji taka nchini China
amerejeshwa kwa mama yake baada ya maafisa wa polisi kubaini kuwa
kutumbukia kwake katika bomba hilo ilikuwa bahati mbaya.
Tukio
hilo la kuokolewa kwa mtoto mchanga katika jimbo la Pujiang lilizua
shutuma kali kutoka kwa raia wa China na wahisani wengi walijitokeza
kumsaidia mtoto huyo wa kiume.
Mtoto huyo tayari amechukuliwa na mama yake kutoka hospitali.
Mwanaume
mmoja ameomba uchunguzi wa kubaini kama mtoto huyo ni wake na kusema
ikibainika ni hivyo, yuko tayari kujadiliana na mama huyo jinsi ya
kumlea.
Polisi wameamua kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 hatakabiliwa na mashitaka yoyote.
Mtoto aliyeokolewa kutoka kwenye bomba la kupitisha maji taka baada ya kupatiwa huduma ya kwanza. |
Source. Mo Blog
No comments:
Post a Comment