Shirika la
Habari la Kimataifa la Uingereza (BBC) lina mpango wa kuhamishia kituo chake
cha redio ya Kiswahili pamoja na kitengo cha uzalishaji wa maudhui ya mtandao
wa BBC Swahili Afrika Mashariki.
Mkurugenzi
wa BBC Global News Peter Horrocks anatarajiwa kutembelea Nairobi kuja kutangaza
mpango huo wa kuhamishia kitengo hicho Afrika Mashariki pamoja na uamuzi wa
kuileta timu nzima ya BBC Swahili karibu zaidi na wasikilizaji wake wa Afrika
Mashariki.
Alisema kila
wiki kumekuwa na ongezeko la watu milioni 20 wanaosikiliza BBC Swahili na idadi
ya watu wanaotembelea mtandao wa Bbcswahili.com wamekuwa wakiongezeka mwaka
hadi mwaka hivyo kuhamishia timu hiyo Afrika Mashariki kutakidhi mahitaji ya
watu hao.
Baada ya
kukamilika mpango huo, utengenezaji wa vipindi vya Kiswahili vya ‘Amka na Bbc’
utahamishiwa Dar es Salaam Tanzania na kipindi cha mchana Dira ya dunia
kitakuwa kikiandaliwa Nairobi, Kenya. Na Uandaaji wa habari za mtandao zitakuwa
zikifanywa sehemu zote mbili Dar es Salaam na Nairobi.
No comments:
Post a Comment