Mkurugenzi wa Taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa Joseph Goliama (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) |
Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Urejesho wa Maadili ya Taifa (Taumata)
iliyosajiriwa kwa usajiri namna S.A 18827, imesisistiza kuwa kurejea katika
maadili mema ndio ufumbuzi wa matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa nasio
vinginevyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam mkurugenzi wa Taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa ndugu Joseph
Goliama alisema kutoka katika maadili mabaya na kuingia katika maadili mema
ndio ufumbuzi wa matatizo ya Taifa kwa sasa.
Alisema kuwa makundi mbalimbali ya wananchi
kuacha maadili mema ya Taifa ndio kumekuwa
msingi chanzo na kiini cha Taifa kupoteza Sauti moja ya kuisikiliza na
mwelekeo mmoja wa kuufuata hali inayosababisha makundi mbalimbali ya wananchi
kutokuwa na amani kutopendana na kutokuaminiana.
Goliama alisema kuwa maadili mabaya ambayo
yanafanya Taifa kupoteza amani, umoja na mawasiliano ni pamoja na makundi
mbalimbali ya wananchi kuwaziana mabaya, kutazamiana mabaya, kuneneana maneno
mabaya, kutendeana mabaya, kuonana kwa jicho baya,kuhusiana kwa uhusiano mbaya,
kufanyiana maamuzi yasiyo ya haki na kusimamiana kwa misimamo isiyo ya haki.
Tunawashauri watanzania wa makundi yote
kurudi katika maadili mema na kuacha maadili mabaya ambayo yanatishia ustawi na
maendeleo ya Taifa letu alisema Goliama.
Alitoa mfano na kusema maadili mabaya ndio
yametumbukiza mataifa mengi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe hivyo akawataka
wananchi wa makundi yote kulinda na kutetea maadili mema ambayo yameifanya
Tanzania kuitwa kisiwa cha amani.
Aliitaka serikali kuangalia uwezekano
wakuyakutanisha makundi yote ya wananchi nakuyakalisha pamoja ili yakubaliane
ni Taifa gani yanataka kulijenga litakalohakikishia kila kundi ustawi na
maendeleo endelevu .
Akifafanua zaidi alisema wadau wa amani na
umoja wa Taifa ni wananchi wa makundi yote yakiwemo makundi ya dini, vyama vya
siasa, jinsia, rika, wafanyabiashara, wafugaji, wakulima, wafanya kazi ,Askari
nakuyataka makundi hayo kupigania amani na umoja na haki ili Taifa liapate
ustawi na maendeleo endelevu.
Goliama alimalizia kwa kuitaka serikali
iishirikishe taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa katika majukum yake ya
kutafuta amani ,umoja na mshikamano wa kitaifa
No comments:
Post a Comment