Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya bonanza la waandishi wa habari lililofanyika kwenye uwanja wa General Tyre, Arusha. |
Mwandishi
Wetu, Arusha
Timu ya
Mpira wa pete (netball) ya wanahabari wa jijini Dar es Salaam,Taswa Queen juzi ilitwaa ushindi katika bonanza la nane
la Waandishi mkoa wa Arusha, baada ya kuichapa timu ya chuo cha uandishi wa
habari Arusha Arusha(AJTC) magoli 21-1.
Wakati Taswa
Queen walikitwaa ubingwa kaka zao, TASWA SC , walishindwa kunyakuwa kombe,
baada ya kutoka suluhu na timu ya AJTC katika mchezo mkali wa fainali, ambao
ulisitishwa kutoka na kiza wakati wa mikwaju ya penati timu hizo, zikiwa
zimefungana 1-1.
Kutokana na
matokeo hayo, Meneja wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL), Endrew
Warden alikabidhi Mwenyekiti wa Taswa SC Majuto Omar fedha taslim 200,000 na
meneja wa AJTC Modaha Lucas alikabidhiwa kiasi cha sh 200,000.
Taswa SC, walifanikiwa kuingia fainali baada ya
kuichapa timu ya Radio 5 magoli 3-1 na baadaye kuifungua timu ya Arusha 1-0
katika mchezo mkali wa nusu fainali.
Kwa Upande
wa AJTC, waliingia fainali baada ya kuichapa timu ya Taswa Arusha, 1-0 na baadaye waliwatoa
Sunrise radio kwa penati 11-12 baada ya timu hizo kutoka sale.
Katika
mchezo wa fainali ya mpira wa pete
uliochezwa uwanja wa general Tyre jijini Arusha, Taswa Queen iliicharaza
Taswa Arusha 45-0 katika mchezo wa nusu fainali na kuisambaratisha AJTC ambao
walikuwa mabingwa watetezi kwa mabao 53-1 katika mchezo wa fainali.
Kutokana na
ushindi huo, Taswa Queen walikabidhiwa kikombe na Meneja mauzo wa kampuni ya
Megatrade, Gudluck Kway na fedha taslimu 150,000.
Katika soka
Taswa Dar pia ilifanikiwa kuingia fainali na timu ya AJTC na licha ya kupigiana
mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya kutofungana, mshindi alishindwa
kupatikana kutokana na kiza uwanjani.
Katika
michezo mingine, timu ya ORS kutoka Manyara, ilifungwa na Sunrise 2-1 na baadaye ORS iliwafungua TBL
Arusha goli 1-0 na hivyo kutwaa zawadi ya timu yenye nidhamu.
Mwenyekiti wa
Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo huku
akiwapongeza wadhamini wao, Delina Group of Companies, Said Salim Bakhresa
& Co Ltd (Azam), DRFA na Kassim
Dewji.
Tamasha hilo
la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, liliandaliwa na TASWA Arusha kwa
ushirikiano na kampuni ya Ms Unique na kudhaminiwa na TBL,TANAPA, egatrade,AICC,Cocacola, Pepsi na Wazee Klabu.
No comments:
Post a Comment