OFISI YA WAZIRI MKUU
KITUO CHA UWEKEZAJI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI.
Kituo cha Uwekezaji
Tanzania TIC kinapenda kutoa taarifa kwa Umma kuhusu mafanikio ya Mpango
wa kuwaunganisha Wajasiriamali wadogo na wakati (Business Linkage)na Makampuni
Makubwa ya kigeni (TNC’S) na ya
Kitanzania ambapo kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na
Biashara (UNCTAD) Mpango huo wa kukuza Uwezo wa kibiashara kwa wajasiriamali
kufanya biashara na Makampuni hayo makubwa.
Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC) ni moja Taasisi ya Serikali ilianzishwa chini ya
Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Namba 26 ya mwaka 1997 kwa kuendeleza, kuratibu
na kuwezesha uwekezaji katika Tanzania. Kama sehemu ya jukumu letu, TIC ina
jukumu la kuhamasisha uwekezaji na masuala yanayohusiana na Uwekezaji kwa
Watanzania ili Uwekezaji uweze kuwa na manufaa kwa Watanzania kwa ujumla.
Katika kipindi chote cha Mpango huo Watanzania
wameweza kuongezewa uwezo kwa kupewa fursa mbalimbali za kiutalamu za kuweza
kukabiliana na ushindani na kuwawezesha kufikia viwango vya Kimataifa vinavyohitajika
na makampuni makubwa ili Makampuni hayo yaweze kutumia bidhaa za Kitanzania
badala ya Kuagiza nje Bidhaa hizo.
Mpaka sasa kituo kimeweza kutoa mafunzo hayo ya
Kitaalamu kwa WAJASILIAMALI wapatao 285 katika mikoa ya Dar-es-salaam,
Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya.
Katika Mafunzo hayo zaidi ya MAKAMPUNI MAKUBWA 28
yaliweza kuhusishwa katika kuwajengea
uwezo na kuwaongezea Utaalamu.
TIC pia katika
jitihada zake za kuongeza faida za uwekezaji katika uchumi wa Tanzania pia
walifanya shughuli kuu ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wawekezaji kupata vibali
vyote vinavyohitajika chini ya One Stop Shop na utoaji wa huduma kwa wawekezaji
aftercare.
TIC imeweza kusajili Miradi kadhaa na katika usajili
huo inawasilisha sekta tano zinazoongoza katika kusajiliwa miradi katika
kipindi cha Januari mpaka Juni 2013 ambazo ni sekta ya Uzalishaji viwandani
miradi 138, Utalii miradi 115, Usafirishaji miradi 82 majengo ya biashara miradi
65 na kilimo miradi 23. Jumla ya miradi yote ilikuwa ni miradi 454 na matarajio
yetu ni kuwa mwaka huu tutasajili miradi zaidi.
Katika usajili wa miradi hiyo wawekezaji wa nje
waliweza kusajili miradi 120 , Miradi ya Ubia kati ya wageni na watanzania
ilikuwa ni 92 na miradi ya Watanzania 242 ambayo ni zaidi ya nusu ya miradi
yote.
No comments:
Post a Comment