TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 3 October 2013

Kampuni Ya Garmin Imeteua Car and General kama Mwenezi wa Afrika Mashariki

Kampuni ya Garmin inafurahia kutangaza uteuzi wa Car and General kama mwenezi wake wa Afrika Mashariki.  Kampuni ya Car and General imekuwa ikiendesha biashara zake katika eneo la Afrika Mashariki kwa muda mrefu huku ikiwa maarufu kwa uuzaji wa nembo kama vile Cummins, Briggs na Stratton, TVS, LML, Champion, Piaggio, Suzuki, Mariner, Electrolux, Ferodo, Ingersoll Rand na Eutectic Castolin katika himaya  11 za  Afrika Mashariki, ambazoni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Uhabeshi, Eritrea, Jibuti, Ushelisheli, Somalia na Sudan Kusini. Car and General waliteuliwa kwa msingi wa ustadi wao wa kutoa usaidizi wa ubora ambao wateja wa Gamin wamekuwa wakifaidika nao kote ulimwenguni.

 
“Tunafurahia sana kutangaza uhusiano huu na tunakaribisha Car and General katika familia ya Garmin”, alisema Walter Mech, Meneja Mkuu wa Gamin katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara. “Uhusiano huu utaimarisha uwepo wa Gamin katikia eneo hili linalokuwa kwa haraka na tuna matumaini ya kufanya kazi kwa karibu na washirika na  wateja wetu katika eneo la Afrika Mshariki.
 
Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1989, Garmin imeweza kuuza vifaa vinavyotumia GPS zaidi ya milioni 100 - hii ni zaidi ya kampuni zote zinazojihusisha na uuzaji wa mitambo ya kuashiria dira. Kampuni ya Gamin ndiyo inayoongoza duniani katika utaalamu wa kuashiria dira kwa kutumia setilaiti, kwa uvumbuzi wa vyombo hivi, Garmin imeweza kuwa katika ulingo wa mbele katika masoko yote inayojihusisha nayo kama vile usafiri kwa magari na rununu, usafiri angani, usafiri baharini, michezo na burudani za nje.
 
Suluhisho la GPS Afika Mashariki linajumuisha vifaa vya mkononi vinavyotumiwa nje ambavyo vimetengenezwa kutumika katika ukulima, uchimbaji madini, uchoraji wa ramani, uvuvi wa kudumu, uhifadhi wa wanyama pori na nyinginezo. Vifaa vyote vya Garmin vinavyotumiwa nje vina mitambo ya GPS yenye uwezo mkubwa wa unasaji na pia uwezo wa kuweka alama za njia. Garmin ina MKD (Mtambo wa kuashiria dira) sahihi kwa soko hili kwani itawasaidia wateja kuweka mipaka ya mashamba yao, kupanda na kuvuna mazao, kuweka alama katika sehemu bora zaidi za uvuvi au hata kuitumia kama kifaa cha kujilinda dhidi ya uwindaji haramu.
 
Garmin pia ina suluhisho la kuwezesha uendeshaji mzuri wa gari barabarani. Kifaa kijulikanacho kama Nuvi kina mtambo wa GPS ambayo iliyopakiwa  ramani za kisasa zenye zaidi ya kilometa 204,000 za kuangazia barabara nchini Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nuvi ina uwezo wa kuonyesha dira na hata kutambua majina ya bararara.  Ikiwa na maelekezo ya kupinda na majina ya barabarani,  nuvi ina Alama Muhimu zaidi ya 45,000 zinazoashiria vituo vya kununua petroli vilivyo karibu zaidi, maduka na mikahawa inayopendwa zaidi na mashine za kutoa pesa zilizo karibu. Kifaa cha Bluetooth huwezesha watumiajii kuambatanisha rununu zao na nuvi ndani ya gari hivyo basi wanakuwa na uwezo wa kuendesha gari bila kushikilia kifaa chochote mkononi.
 
“Bila shaka ni ramani yenyewe itakayotiliwa mkazo zaidi Afrika Mashariki na jambo hili litasababisha kuwa na uhusiano baina ya nchi mbalimbali ili kuelewa mahitaji ya watumiaji. Usafiri kwa gari, Vifaa vya kutumiwa nje na pia Usafiri baharini ni mambo yenye umuhimu kulingana na jinsi muundo msingi unazidi kupanuka katika bara la Afrika”, kasema Mech. “Kuingia kwa Garmin Afrika Mashariki ni kwa minajili ya kuhakikisha kuwa, hata ukienda wapi, utakuwa na teknologia ya kisasa ya kusafiri mkononi mwako, hii ikiambatana na usaidizi wa ufundi wa hali ya juu zaidi na mpangilio mzuri wa waranti kwa wateja.”
 
Distributed by the African Press Organization on behalf of Garmin Southern Africa (PTY) Ltd.
 
 
Mwenezi: Gamin South Africa
Mawasiliano: Michelle Hohls
Simu: +27 11 251 9964

No comments:

Post a Comment