Na gazeti la Mwananchi
Wauziwa tiketi za basi ambalo halipo kabisa katika eneo la maegesho ya kituo hicho.
Wauziwa tiketi za basi ambalo halipo kabisa katika eneo la maegesho ya kituo hicho.
Dar es Salaam. Abiria waliokuwa
wasafiri kwenda Korogwe kwa basi (jina tunalihifadhi) wamekumbana na
utapeli wa aina yake baada ya kuelezwa kuwa basi hilo halipo.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi ambalo lilishuhudia baadhi ya abiria wakifika
kwenye ofisi ya basi hilo kutaka kurudishiwa fedha zao huku wengine
wakipigwa butwaa kituoni hapo baada ya kuambiwa basi halipo.
Hata hivyo, mmoja wa abiria alisema kuwa,
walichukua hatua hiyo kutaka kurudishiwa fedha zao baada ya kuona hakuna
dalili za basi hilo licha ya kutakiwa kuripoti saa 4:30 asubuhi.
Akizungumza na Mwananchi, mwanadada ambaye hata
hivyo alisema si msemaji, alidai kuwa gari lao limepata pancha hivyo
haliwezi kusafiri.
Mwananchi ilipohoji pancha hiyo ni ya kiasi gani
mpaka wafute safari, mwanadada huyo alionekana kubabaika lakini
alisisitiza kuwa basi hilo limeshindwa kusafiri kutokana na hali hiyo.
Mmoja wa abiria waliokuwa wasafiri na basi hilo
alisema, utapeli kama huo umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu kituoni
hapo kwa kuwakatia tiketi abiria na kuwaonyesha gari huku wakifahamu
wazi kuwa gari husika halipo na kinachofanyika kesho yake ni kupewa gari
tofauti na makubaliano ya awali.
Mwananchi ilishuhudia abiria hao waliokuwa
wasafiri na basi hilo wakifaulishwa kwenye basi lingine ambalo
halifanani kabisa na lililochapishwa kwenye tiketi za basi
walilotarajiwa kuondoka nalo.
Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida
ikionekana kinachofanyika katika kituo hicho kinafahamika wahudumu wa
basi hilo lililoondoka walizichukua tiketi za basi lililodaiwa kuwa ni
bovu na kuwapa tiketi nyingine na kuendelea na safari. Matukio kama hayo
yamekuwa yakishamiri kituoni hapo hasa mwishoni mwa mwaka.
No comments:
Post a Comment