Na Mwandishi wetu
Bioteknojia ya kisasa ni nyenzo mpya inayoweza kuboresha sekta mbali mbali za kiuchumi zikiwemo sekta za kilimo, mifugo misitu, uzalishaji viwandani, na hifadhi ya mazingira.
Hayo yameelezwa leo
jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula
Katika ufunguzi wa Warsha ya kufunga mradi wa matumizi salama ya bioteknolojia
ya kisasa.
Bw.Salula amesema kuwa,
lengo kuu la teknnolojia hii ni kukidhi haja mbali mbali za binadamu kama vile
kuimarisha ubora wa mazao, kukidhi magonjwa, kupata mbegu za mazao yanayohimili
ukame na kukuza uzalishaji.
Aidha, aliongeza kuwa,
pamoja na faida za bioteknolojia ya kisasa, bado kuna wasiwasi kuhusu athari
zinazoweza kutokea kutokana na bioteknolojia hii ikiwa ni pamoja na uzio yaani allergy, kujitokeza kwa magugu sugu, saratani na usugu katika matibabu ya magonjwa.
Alisisitiza kuwa,
serikali imejiandaa kupunguza na kudhibiti athari hizi kutokana na sababu kuwa
Tanzania, haiwezi kukwepa athari zinazoweza kutokea kutokana na muingiliano wa kimataifa hususan utandawazi
pamoja na mianya iliyopo katika mipaka na kuzingatia umuhimu wa matumizi ya
biteknolijia ya kisasa katika nchi yetu.
"Si kweli kwamba Tanzania inakataa matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa bali tunadhibiti ili
kuepuka madhara yatokanayo na bioteknolojia ya hiyo, Alisisitiza"
Bw. Salula alianisha
kuwa Tanzania kama nchi nyingine ni muhimu ikawa na mfumo na vifaa
vitakavyodhibiti bioteknolojia ya kisasa, ikiwa ni wanachama wa mkataba wa
Cartagena Tanzania inatakiwa kuweka taratibu zitakazo hakikisha matumizi salama
ya bioteknolojia ya kisasa.
Mradi huu ulikuwa na
lengo la kujenga uwezo kwa sekta na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na
bioteknolojia ya kisasa ambapo maabara za taasisi tano zilipatiwa vifaa vya
kisasa vya kusaidia kutambua na kufanya tathmini ya usimamizi angalifu wa
bidhaa za mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki.
Maabara zilizonufaika
na msaada huo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine, Taasisi ya Utafiti na Kilimo - Zanzibar, Taasisi ya Utafiti na Kilimo
- Mikocheni na Mamlaka ya Chakula na Madawa Tanzania.
EVELYN MKOKOI NA LULU
MUSSA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM
13/12/2013
No comments:
Post a Comment