![]() |
| Wachezaji wakiwasili kutoka Malawi walikokuwa na mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Malawi iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Kamuzu Banda. (Picha ni kwa hisani ya Bin Zubeiry) |
Monday, 12 October 2015
Taifa Stars yatua Dar
AY awapongeza Diamond, Vanesa Mdee na Ommy Dimpoz kwa kutwaa tuzo
Katika ukurasa wake wa Facebook, Ambwene Yesaya 'AY' amewapongeza Diamond Plutnumz, Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz kwa kupata tuzo zaAfrimma zilizotolewa Marekani.
Alisema ushindi huo umeipa heshima Tanzania na Afrika Mashariki.
Diamond amepata tuzo tatu kupitia wimbo wake wa Nana wakati Vanesa Mdee kapata tuzo moja na Ommy moja.
Tuesday, 6 October 2015
Sherehe za Shule ya Sekondari Imperial Msolwa Chalinze mwishoni mwa wiki iliyopita.
| Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Imperial iliyopo Msolwa Chalinze |
Ada ni sh. Milioni 10 kwa mwaka.
Nduguye Messi amiliki 'bunduki bila kibali'
BBC SWAHILI
Kakaake mkubwa nyota wa timu ya Argentina na Barcelona Lionel Messi amekamatwa kwa kumiliki bunduki bila kibali.
Polisi wanasema kuwa Matias mwenye umri wa miaka 33 alikataa kuonyesha vibali vyake aliposimamishwa katika mji wa Rosario.
Polisi walilikagua gari lake na kupata bunduki ambayo Matias ameshindwa kutoa kibali chake cha umiliki.
Maafisa hao wanasema kulikuwa na mvutano kati yao na ndugu huyo wa Messi ambapo alijeruhiwa katika jicho huku maafisa hao wakipata majeraha madogo.
Baadaye alipelekwa katika kituo kimoja cha polisi mjini Rosario na kuzuiliwa kwa kwa saa nne.
Alikamatwa mara moja kabla ya mwaka 2008 kwa kubeba silaha bila kibali.
Watu wa familia ya Messi pia wanakabiliwa na madai ya kukwepa kulipa kodi nchini Uhispania.
Lionel Messi na babaake Jorge wote wanatuhumiwa kuiibia mamlaka zaidi ya yuro milioni 4 zinazohusishwa na mapato kutokana na matumizi ya jina lake.
Tuzo za Taswa Oktoba 12
Sherehe za utoaji tuzo kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwa miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete sasa zitafanyika Oktoba 12 badala ya tarehe iliyotangazwa awali.
Taswa licha ya kutoa tuzo kwa wachezaji
waliofanya vizuri zaidi, pia itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake katika michezo wakati
wa uongozi wake.
Baadhi
ya mambo hayo ni serikali yake ilivyolipia makocha wa michezo ya soka, netiboli na ngumi
na pia serikali ilipeleka wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa
maandalizi ya mashindano ya kimataifa.
Pia serikali yake ilirejesha michezo shuleni
pamoja na mashindano ya michezo kwa shule za msingi na sekondari (UMITASHUMTA
na UMISETA).
Pia tukio hilo la tuzo itakuwa sehemu ya
wanamichezo kumuaga Rais Kikwete ambaye anamaliza muda wake kikatiba baada ya
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Maandalizi muhimu kwa tukio hilo yamekamilika
ikiwa ni pamoja na kupata majina ya wanamichezo hao watakaopewa tuzo siku hiyo.
Alhamisi wiki hii Taswa itatangaza wadhamini
wengine watakaoungana na wadhamini ambao tayari wametangazwa ambao ni GSM
Foundation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Ahsnateni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
05/10/201
Sports journalism program accepting applications [Worldwide]
IJNET
Student journalists from around the world can apply for the program.
The World Curling Federation (WCF) is accepting applications for its sports media trainee program. Eight students will be selected to be immersed in the journalism, photography and TV production departments of the 2015-2016 curling championships.
One journalism trainee and one photography trainee will travel to Le Gruyère European Curling Championships Nov. 20 to 28, 2015 in Esbjerg, Denmark.
One journalism trainee, one photography trainee and a TV production trainee will intern at the World Junior Curling Championships March 5 to 13, 2016 in Erzurum, Turkey.
And a trainee in each of the three disciplines will cover the World Mixed Doubles Curling Championship April 16 to 24 in in Karlstad, Sweden.
The selected students will receive a fully paid trip to the championships, accommodations and some living expenses for the duration of the events.
The application deadline is Oct. 20.
For more information, click here.
Student journalists from around the world can apply for the program.
The World Curling Federation (WCF) is accepting applications for its sports media trainee program. Eight students will be selected to be immersed in the journalism, photography and TV production departments of the 2015-2016 curling championships.
One journalism trainee and one photography trainee will travel to Le Gruyère European Curling Championships Nov. 20 to 28, 2015 in Esbjerg, Denmark.
One journalism trainee, one photography trainee and a TV production trainee will intern at the World Junior Curling Championships March 5 to 13, 2016 in Erzurum, Turkey.
And a trainee in each of the three disciplines will cover the World Mixed Doubles Curling Championship April 16 to 24 in in Karlstad, Sweden.
The selected students will receive a fully paid trip to the championships, accommodations and some living expenses for the duration of the events.
The application deadline is Oct. 20.
For more information, click here.
Stanford fellowship for democracy, development open [Worldwide]
IJNET
Journalists involved in their country's economic and political development can apply for a summer fellowship at Stanford University.
The Draper Hills Summer Fellowship on Democracy and Development is a three-week program that brings together 25 to 30 midcareer professionals in the field of democracy, development and the rule of law, especially those from developing countries.
The 2016 program will take place July 17 to Aug. 5 in Stanford, California. The fellowship provides a forum for emerging leaders to connect, exchange experiences and receive academic training through seminars, academic readings and classroom-based curriculum.
The university covers travel, accommodation, living expenses and visa costs.
The deadline is Nov. 18.
For more information, click here.
Journalists involved in their country's economic and political development can apply for a summer fellowship at Stanford University.
The Draper Hills Summer Fellowship on Democracy and Development is a three-week program that brings together 25 to 30 midcareer professionals in the field of democracy, development and the rule of law, especially those from developing countries.
The 2016 program will take place July 17 to Aug. 5 in Stanford, California. The fellowship provides a forum for emerging leaders to connect, exchange experiences and receive academic training through seminars, academic readings and classroom-based curriculum.
The university covers travel, accommodation, living expenses and visa costs.
The deadline is Nov. 18.
For more information, click here.
Mkwasa apewa mkataba wa kudumu Stars
| Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Charles Mkwasa |
Kocha wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Charles Mkwasa amepewa mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika Machi 31, 2017.
TFF Imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa baada ya kurudhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.
Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.
Naye kocha Mkwassa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda.
Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.
Stars yakamilika kuivaa Malawi kesho
| Kocha wa Timu ya Taifa Stars Charles Mkwasa (Kulia) na Kocha wa timu ya taifa ya Malawi 'The Flames' Ramadhan Nsanzurwimo |
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema kikosi
chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kwa
Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
Mkwasa amesema kikosi chake kipo kaika hali nzuri baada ya kufanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ambapo wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakiwemo wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kutoka klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.
“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa kesho, wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu, kikubwa tunawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutu sapoti katika mchezo huo wa kesho” Alisema Mkwasa.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa Malawi (The Flames), Ramadhan Nsanzurwimo amesema wanaiheshimu Tanzania, wanatambua kesho kutakua na mchezo mzuri, na wao kama Malawi wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo.
Friday, 2 October 2015
Walimu 245,000 kukosa mshahara Kenya
BBC SWAHILI
Zaidi ya walimu 245,000 hawatapata
mishahara yao mwezi huu,kufuatia mgomo wa nyongeza ya mishahara
unaondelea kwa wiki ya sita sasa kulingana na gazeti la nation nchini
humo.
Siku ya Alhamisi mahakama ya rufaa iliwagiza walimu kurudi shuleni mara moja huku ikiwa mamilioni ya watoto wa shule hawaezi kwenda shule kutokana na mgomo huo.
Mahakama ya Kenya imeiagiza serikali kuongeza mishahara ya walimu kwa hadi asilimia 50,lakini serikali inapinga hilo ikidai kwamba haina fedha za kuwalipa.
U15 Yaichapa Kombaini Tanga 4-0
Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (U-15) jana imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu, baada ya kuichapa mabao 4-0 kombaini ya U-15 ya Tanga Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ushindi huo umetokana na mabao mawili ya Issa Abdi dakika ya 21 na 23, Frank George dakika ya tisa na Ibrahim Abdallah Ali dakika ya 80.
Pamoja na ushindi huo, lakini vijana wa U-15 ya Taifa walikutana na ushindani kutoka kwa wachezaji wenye vipaji wa U-15 ya Tanga.
Kivutio zaidi alikuwa ni kiungo Joseph Yakobo ambaye Tanga wanamuita ‘Sure Boy’ na mshambuliaji George Chande aliyeisumbua mno ngome ya timu ya taifa iliyoongozwa na Nahodha, Maulid Lembe.
Wednesday, 30 September 2015
TASOI yazindua Kampeni ya Saratani kwa kutumia Teknolojia ya Mawasiliano
Katibu
Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati endelevu wa kuendesha
kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia technolojia ya
mawasiliano katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani
Ocean Road leo jijini Dar.
Daktari bingwa wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Dominista Kombe(Kulia) akitoa takwimu ya wagonjwa wanaofika kutibiwa katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Kinga Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage
akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati
wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean
Road leo.
ASASI
isiyo ya kiserikali ya Tanzania Social Outreach Initiative (TASOI),
imezindua kampeni rasmi mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya
Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo, alisema
kuwa kampeni hiyo itatoa elimu, uhamasishaji na kutoa ushauri nasaha
kwa wananchi kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS).
Ng'anyagwa kufanya ziara miji 10 Tanzania
| Mwanamuziki wa muziki wa Reggae Innocent Ng'anyagwa akiimba kwenye jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) hivi karibuni. |
Nyota wa muziki wa Reggae Innocent Ng'anyagwa maarufu kama Ras Inno anatarajia kufanya onesho Mbeya Oktoba 10, Songea Oktoba 17 na kwenda kwao Iringa. Pia, atafanya ziara Dar es Salaam, Kahama na Arusha.
Ziara hiyo ni kutangaza albam yake ya Love Story na kusaidia makundi maalum na kuibua vipaji vya wasanii chipukizi wanaopenda muziki huo.
Ras Inno alisema ili kukamilisha ziara hiyo anaomba wadau mbalimbali, Taasisi na Makampuni kumuunga mkono.
Tuesday, 29 September 2015
Taarifa ya Mbeya City kuhusu Nyoso
Bodi ya klabu ya Mbeya City ilikutana jana tarehe 29.09.2015 kwa dharura kulijadili suala ambalo hivi sasa linaendelea kujadiliwa katika Umma wa wanamichezo nchini likimuhusisha mchezaji wa timu yetu Juma Said maarufu kama “Nyoso” baada ya mchezo kati ya timu yetu na Azam Fc uliochezwa tarehe 27.9.2015 katika uwanja wa chamanzi.
Katika kikao hicho kilichomalizika hivi punde,yafuatayo yameamuliwa
Kwa kuwa katibu Mkuu wa Klabu jana aliiagiza idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Klabu kulifanyia utafiti suala hili,Bodi imeiongezea idara hiyo wajumbe wawili ili kuunda kikosi kazi kitakachofanya kazi kwa adidu za rejea zifuatazo:
(a) Kupitia rejea za mchezo husika na kuangalia Mazingira na Asili ya suala zima lililojitokeza.
(b) Kupata Maelezo ya awali ya mchezaji wetu juu ya suala lenyewe.
(c) Kufanya uchambuzi wa kisayansi wa mzizi wa suala analohusishwa mchezaji kwa kushirikisha watalaam wa Ushauri Nasihi na Saikolojia kisha kuishauri Bodi.
2. Kazi hii iwe imekamilika ndani ya masaa 86 kuanzia jana saa saba mchana ilipoanza.
Klabu inaomba umma wa wanumma wa wanamichezo kuwa na subira.
Kazi hii iwe imekamilika ndani ya masaa 86 kuanzia jana saa saba mchana ilipoanza.
Klabu inaomba umma wa wanamichezo kuwa na subira.
Wasalaam,
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
Nyoso afungiwa miaka miwili
| Juma Nyoso |
Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana jana kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.
Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
